2017-05-13 15:34:00

Papa Francisko ni Askofu kati ya Maaskofu kuongoza Kanisa la Mungu


Baba Mtakatifu Francisko anafanya nini cha kuvutia?: Je hiyo si suala la mtindo wake, unyenyekevu wake na ukweli wake au ombi lake la unyenyekevu , au mag’amuzi  na huduma, juhudi zake kuhusu  maskini na wanyonge. Yeye anataka kuanzisha kwa dhati mageuzi ya kweli katika Kanisa  ambayo ndiyo msingi wa utume halisi wa kanisa  Hayo yamesema na Askofu Mkuu Brian Farrell  Katibu wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha umoja wa Wakristo wakati wa hoba yake tarehe 12 Aprili 2017 huko  Castel Gandolfo Roma. Ni  katika mkutano wa wiki moja wa kiekumene iliyoandaliwa na Chama cha Wafokolari  ikiwa na kauli mbiu "tutembee pamoja.Wakristo kulekea umoja". Monsinyo Farrell amesema, Baba Mtakatifu  Francisko akilini mwake yapo mageuzi ya kipapa na kiaskofu akiwahutubia umati wa watu 700 kutoka katika Makanisa 69 na jumuiya za kikristo  kutoka  nchi 40 za dunia.

Aidha amesema; kuhusu utekelezaji wa huduma ya kipapa, Baba Mtakatifu Francisko anaamini kuwa Papa mwenyewe hana nafasi ya juu zaidi ya Kanisa bali yeye ni Askofu kati ya maaskofu wengine ambaye anaitwa kuwa khalifa wa Mtakatifu Petro, kuliongoza Kanisa la Roma lakini ambaye analiongoza Kanisa katika upendo  wa makanisa yote ulimwenguni. Askofu Mkuu  Farrel anaongeza kwamba, kwa upande wa maaskofu duniani, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika mara nyingi kuwajibika  wakiwa wa kwanza katoa huduma ya kichungaji. 

Aidha anaeleza, hatua hizi zote ni zoezi kwa mfumko kuanzia utawala Mkuu wa Kanisa  kuelekea katika Kanisa mahalia ambapo ufanya kuwa  sehemu ya roho ya  umoja ambayo inajikita katika jukumu lake chini ya sheria kuu ya upendo, mshikamano undugu na uwajibikaji wa pamoja. Kwa maana nyingine, Askofu Mkuu Farrell, anaongeza kwa kifupi Baba Mtakatifu yupo anatafuta tofauti na mapana ya uwiano wa majukumu na mamlaka ya Kanisa , yaani muungano halisi wa umoja na mshikamo, kwa njia ya kiekuemene duniani  ambayo  kwa hakika inaweza kuleta mageuzi ndani ya Kanisa Katoliki, na kwamba ni muhimu kwasababu ya matumaini katika karne ya 21 ya kurudisha umoja kamili wa nchi za mashariki.

Kwa kumalizia hotuba yake katika mtazamo wa kiekumene amesisitiza kwamba Kanisa leo hii bado linahitaji karama  ya umoja kama ile ya Chiara Lubich, kuhusiana na roho ya umoja ambayo ndiyo kauli mbiu ya shirika hilo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.