2017-05-13 15:58:00

Mongolia: Kanisa linaadhimisha Jubilei ya miaka 25 ya umisionari!


Ni hatua ya kihistoria katika Kanisa la Mongolia na  Ubalozi wa Kitume wa Ulaanbaatar kwasababu ya kuadhimisha matukio mawili kwa pamoja. Kwanza ni kutimiza miaka 25 ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Vatican na jamhuri ya nchi ya Mongolia; pili ni  sikukuu ya  maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Kanisa Katoliki katika nchi hiyo.  Aliyasema hayo  Askofu Mkuu Wenceslao S. Padilla Balozi wa Kitume wa Papa huko Ulaanbaatar Mongolia  akihojiwa na Shirika la habari za kimisionari katoliki na pia mmisionari mmoja kutoka Afrika  padre  Prosper Mbumba ambapo Kanisa hilo linakadiiriwa na  idadi ya wakatoliki walio batizwa 1300 huko Mongolia. 

Hata hivyo Kanisa la Mongolia linahesabu mamia ya wakatekumeni kutoka katika maparokia 6 na vituo 3 vya kimisionari  ambapo katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 wanafungua parokia mpya. Kwa sasa wamisionari wa kike na kiume 50 kutoka katika nchi 14 za dunia.  Padre  Prosper Mbumba amaaye anatoa huduma katika maisha ya Mongolia anasema; wakristo kwa dhati wanajikita katika kuhamasisha wito wao na kujenga uhusiano wa kina na Mungu  kwa  kujitoa sadaka kuwasaidia wengine.

Wakati wa kujiandaa na tukio la Jubilei  ya miaka 25 iweze, Kanisa mahali wameandaa shughuli tofauti ili kuweza kufikia kilele katika hali yenye mwanga zaidi kwa kipindi cha  maisha ya utume wa Kanisa la Mongolia. Kati ya shughuli hizo ni semina ya kiteolojia juu ya utume, semina iliyoanzia tarehe 8 hadi 12 Mei 2017. Maandalizi ya semina hiyo yameandaliwa  na Baraza la Kipapa la Umoja wa Wamisionari. Semina hiyo imejadili mada mbalimbali na miongoni mwa mada hizo ni pamoja na  roho ya kimisonari  katika bara la Asia ya sasa; historia ya Yesu kama msingi wa utume na mazungumzo ya kidini katika utume wa uinjilishaji wa Kanisa. 


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.