2017-05-12 17:12:00

Salam na matashi mema kwa Papa kutoka kwa Rais Sergio Mattarella


Rais Sergio Mattarella wa Italia, Ijumaa, tarehe 12 Mei 2017 amemwandikia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa shukrani kwa salam na matashi mema aliyomtakia binafsi na kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Italia, wakati akiwa njiani kuelekea Fatima, nchini Ureno kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Bikira Maria alipowatokea Watoto wa Fatima.

Kwa njia ya hija hii ya kitume, anasema, Rais Mattarella, inakuwa ni mwaliko wa amani na matumaini kwa familia yote ya binadamu; inayofumbatwa katika dhamana ya uwajibikaji na akili kwa watu wote wenye mapenzi mema, ili kujikita katika ujenzi wa dunia inayosimikwa katika haki. Anamshukuru Baba Mtakatifu kwa matashi na baraka zake kwa wananchi wote wa Italia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.