2017-05-12 16:43:00

Matumaini mapya ya Korea ya Kusini baada ya uchaguzi wa Rais mpya


"Wazalendo wa nchi yetu wamemkabidhi Rais mpya  majukumu makubwa. Ninaomba sala zangu  kwa Mungu ili aweze kupata nguvu na hekima ya kukabiliana na changamoto inayokumbana nazo za nchi ya Korea Kusini". Ni maneno kutoka katika ujumbe wa Kardinali Andrew Yeom Soo-Jung, Askofu Mkuu wa Seoul akilezea juu ya uchaguzi wa Rais mpya wa Corea ya Kusini, Moon Jae-in hivi karibuni.Ni matashi  mema kwa namna ya pekee ili kwamba Rais mpya wa Serikali anambaye ni Mkatoliki, mwakili na mtetezi wa haki za binadamu anaweza kutetea haki, amani na mshikamano kwa wema wa nchi na zaidi kuwatetea na kuwalinda walio wadhaifu. 

Katika mahojiano na Shirika la Habari la Sir Askofu  Lazzaro You Heung-sik  wa Jimbo la Daejeon, amesema kuwa, anayo furaha kubwa kuona kwamba sasa nchi ya Korea Kusini inaweza kugeuza ukurasa na kuanza historia mpya. Kuhusiana na uchaguzi huo, Askofu anasema wazalendo wa Korea wamasema inatosha sasa na kupiga kura kwa ajili ya kusahau yale yote yaliyo pita. Anaongeza; nchi ya Korea imepitia katika kipindi kigumu cha migogoro.Ni kipindi kilicho jionesha wazi kwenye kashfa na kesi za rushwa iliyohusisha hata rais wa zamani Park Geun-hye vilevile kuanguka chini viwanda vikubwa vya nchi. 

Kuhusiana na uhusiano kati ya Korea ya Kaskazini amesema, uchaguzi wa Rais Moon Jae-in unatia  matumaini kwa sababu kwa miaka ya hivi karibuni, mahusiano ya nchi mbili hizi za Korea umekuwa wenye matata. Kwa sasa ni lazima kutafua njia mpya ya mazungumzo na mahusiano ili kutambua namna ya kuishi pamoja kwa amani. Kwa njia hiyo ni matumaini yao kutokana na tamko la kwanza alilosema Rais mpya kuhusu uhusiano wa Washington na hata Pyongyang baada ya siku chache za mvutano.Wakati wa hotuba yake ya kwanza  Rais mpya wa Korea ya Kusini alisema "Kama ni lazima ningependa kuruka Washington mara moja" na "hata  Beijing na Tokyo."

Katika  mazungumzo muhimu ya kukomesha viitisho cha nyuklia, Rais mpya wa Korea ya Kusini amesema yuko tayari kwenda iwapo kuna ulazima hata Pyongyang. Aidha Askofu Daejeon amesisitiza, ni muhimu sana Korea ya Kusini sasa isianze  tena kwa upya  mvutano, bali itumie nafasi hiyo kufanya mapatano hata katika ngazi ya kimataifa kwa kushiriki kujenga madaraja ya amani katika nchi za Bara la Asia na dunia kwa ujumla.

Askofu Daejeon ameelezea pia  kuhusu kipaumbele ambacho wanatarajia kutoka kwake Rais mpya wa nchi yao kwamba,Rais anapaswa lakini  ni mtu aliye wazi , hivyo awe mwajibikaji kwa kujikita zaidi katika juhudi kwa ajili ya wote; awe mwenye uwezo wa kutengeneza hali na matumaini kwa raia wake pamoja na mazungumzo na watu wote wa nchi. Kwa njia hiyo ni lazima kufungua njia mpya ili kuweza kuelekea katika njia za mazungumzo na mapatano kwa kutafuta ufumbuzi wa kuishi kwa amani katika nchi ya Korea kusini na Kaskazini.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.