2017-05-12 15:43:00

Fadwa Barghouti atetea wafungwa wa kipalestina kwa ujumbe muhimu!


Mwanasheria Fadwa Barghuthi mke wa Kiongozi wa kipalesitina Marwan Barghuthi anayeongoza mgomo wa kususia chakula kwa wafungwa 1800 wa kipalestina katika Magereza nchini Israeli ametuma Barua kwa Baba Mtakatifu Francesko  akiomba aingilie katika masuala ya wafungwa wa kipalestina kabla hawajachelewa. Habari hizi zimetolewa na Balozi wa Kipalestina nchini Italia tarehe 11 Aprili 2017 kwamba, ujumbe wa wito wake umekabidhiwa katika mamlaka Katoliki ya Kipalestina wakati wa mkutano uliofanyika Ramallah. Wito huo unakumbusha kwamba uhuru na adhi ya mtu ni zawadi kutoka kwa Mungu ambapo hakuna kikundi cha aina yoyote ya  kibinadamu aweza kuzuia mwingine haki hizo.

Mke wa Marwan  kwenye ujumbe wake aliotuma  Baba Mtakatifu Francisko anatoa sababu zinazowafanya wafungwa 1800 kufanya uamuzi wa kususia chakula ambapo sasa ni siku 25 zimepita wakionesha jinsi gani nchi ya Israeli inakiuka haki zao. Ni tendo la nguvu kwa upande wao kuendelea kuhamasisha madai ya msingi ambayo ni halali na haki ya wana familia kuwatembelea wafungwa hao, haki ya elimu, halikadhalika kukomesha vitendo vya kiholela vya kutoa adhabu, mateso na dhuluma, na ukosefu wa kukusudia katika uzembe wa kutoa huduma ya afya dhidi ya wafungwa.

Kwa upande wa wafungwa kama anavyo ripoti  mke wa kiongozi huyo Barguthi ni waathirika wa adhabu ya pamoja kutoka mamlaka ya Israeli na wameachwa na dunia. Ikumbukwe kwamba Marwan Barghuth ni mwanachama wa Al-Fatah  na mbunge wa Kipalestina ambaye yuko jela kwa miaka 15 kwa tuhuma kutoka nchi ya  Israel kuwa ni gaidi na mmoja wa kuwajibika na mauaji ya raia wa Israeli. Barghuthi daima amekanusha mashitaka hayo na kwamba hana hatia, hata katika machakato wa kesi yake alikataa kujitetea kwa sababu ya kutambua hana hatia katika mahakama ya Israeli.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.