2017-05-11 08:45:00

Italia:Maelfu ya wanafunzi katika Siku ya XXII ya Amani Pompei


Tarehe 10 Mei 2017 katika mji wa Pompei nchini Italia kumefanyika maandamao ya XXII ya siku ya Amani  kwa wanafunzi wa Mji wa Pompei. Siku hiyo imeongozwa kwa  kauli mbiu  "kutotumia nguvu mtindo wa maisha" ambao ni Ujumbe wa Baba  Mtakatifu Francisko wa Siku ya Amani duniani kwa mwaka huu:Ni ujumbe ambapo unataka  dunia iweze kujifunza kwa upya  kutotumia nguvu na ndiyo uwe mtindo wa maisha ya kila mtu binafsi, jamii yote hadi mipaka yote ya dunia.

Ni tukio lilowaunganisha wanafunzi zaidi ya 3000 ambapo wameandamana kwenye  barabara wakipeleka ujumbe  wa amani. Ni wanafunzi kutoka shule za aina mbalimbali za Mji wa Pompei  na mipaka yake ambapo maandamano hayo yamewafikisha katika uwanja wa Madhabahu ya Kipapa ya Mama Maria wa Rosari wa Pompei wakiwa wanaongoza na Band mbalimbali za mjini kama vile ya Bartolo Longo, Maaskari Gereza na nyinginezo nyingi za mji wa Pompei. Aliyefungua maandamano ya XXII ya amani na kuwakaribisha ni Fratelii Filippo  Risso wa Shirika la Ndugu wa Mashule ya Kikristo ambaye ni Mkurugenzi wa wa Kituo cha Bartolo Longo mjini Pompei na  mwandaaji wa maandamano ya amani kwa ajili ya vijana. Katika Hotuba yake amasema hawa ni maelefu ya vijana  karibia 3000 ambao ni wajenzi wa amani na katika kila moyo wa mtoto anayo amani ndani yake, inayopaswa pia kulindwa na kuitetea kwa ajili ya wote duniani kote.

Aidha naye  Askofu Mkuu na Msimamizi wa Kitume katika Madhabahu ya Pompei Thomas Caputo, ameshiriki maandamano hayo pia katika kutoa hotuba yake  amewaalika wafuate maneno  na ushauri wa Baba  Mtakatifu Francisko kila wakati na zaidi wajifunze kuwa watu wa amani. Amesema hiyo ikiwa ni kwa ajili ya  mkubwa na mdogo  watafakari amri kumi za Bwana kwa kujikita kiundani zaidi na kuziweka katika matendo ya kila siku kutoka katika Injili nzuri ya Mtakatifu Matayo.

Maombi yalifuatia yaliyo andaliwa na wanafunzi wenyewe  kwa msaada wa walimu wao ambapo yalikuwa yanalenga juu ya  ndoto ya amani miongoni mwa kila mtu duniani lakini zaidi kwa vijana na watoto ambao ndiyo wako mstari wa mbele pia fursa  kubwa katika kujikita kwenye ujenzi wa amani. Kadhalika wanasema  dunia ikiwa na amani inaweza kuruhusu kila mtu kuondokana na uchungu,mateso na manyanyaso na zaidi kutoa fursa ya kuruka bila mabawa katika kueneza amani  kwa wengine na uhuru. Aidha maombi ya amani kwasababu inatoa furaha ya moyo ili kuwasambazia watu wengine wenye mahitaji.

Maandamano yamemalizika na ishara ya kuwaachia huru njiwa wengi waruke hangani  na pia kuweka taji la mawaridi katika sanamu ya Mama. Jambo zuri la kufurahisha  limekuwa la  kurusha mawaridi kutokea juu ya Kinara cha Kengele ya Madhabau ya Mama Maria wa Pomepei.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.