2017-05-10 14:38:00

Laterano wafanya Mkutano wa Mafundisho Jamii ya Kanisa 16-17 Mei


Tarehe 16 na 17 Mei 2017 Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano  Roma kutafanyika Mkutano ambao ni wa kila mwaka kuhusu Mafundisho jamii  Kanisa ulio andaliwa na sehemu ya Kimataifa katika  utafiti kuhusu Waraka wa "Ukweli katika Upendo (Caritas in Veritas) katika  Chuo  hicho kwa kuongozwa na Flavio Felice kwa ushirikiano na Kiti cha Yohane Paulo II; Falsafa na historia ya Taasisi mbalimbali za Ulaya ikiongozwa na Rocco Buttiglione; Mizizi ya kikristo na uzalendo wa Ulaya kwa  miaka 60 ya Mkataba wa Roma. Hizi ndizo mada kuu zilizochaguliwa kwa siku hizo mbili zikiwa zinalenga hali halisi ya sanaa na matarajio ya mafundisho jamii ya Kanisa pamoja na kujadili  maisha endelevu ya Ulaya.

Miongoni mwa masuala makuu yatakayoshughulikiwa  katika njia ya taaluma mbalimbali ni pamoja na kutazama "ulinzi na heshima  ya binadamu na mtazamo wa utu wa sasa katika mikataba; aidha uchumi jumuishi zaidi ambao  unaelekeza  manufaa ya wote, hasa kwa kuzingatia uchumi wa kijamii na huru wa kimasoko.

Taarifa pia zinasema ni kuweka mtazamo kwa undani zaidi wa Ulaya katika siku zijazo ambapo inaonesha wazi mabadiko mengi ambayo hayajawahi kutokea hapo hawali.Kwa njia hiyo ni kutaka kugundua kwa upya thamani yake, pamoja na matumaini ya  mabadiliko ya kweli kwenye hatua za haraka. Aidha wataangalia na kuchambua  kazi iliyofanyika ya mwisho kwa kushirikiana na Kamati ya Kisayansi na waratibu wa Siku ya 48 ya wiki jamii Katoliki Italia.

Sr Angela Rwezula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.