2017-05-10 14:16:00

Kard.Onayeiyekan:Serikali ya Nigeria ilisubiri nini miaka mitatu?


Tumshukuru Mungu kwasababu ya wasichana  kuweza kuwakumbatia familia zao, lakini najiuliza kwanini walisumbiri hadi miaka mitatu jambo hili kufanyika?.Ni swali lake Kardinali John Olorunfemi Onayeiyekan ,Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Abuja akijadili kuhusu kuachiwa huru wanafunzi wasichana  82  waliokuwa wametekwa nyara na Boko Haram katika shule yao Chibok tarehe 14 Aprili 2014.
Kardinali anasema kwa njia ya Gazeti la Fides kwamba; kwa miaka yote hiyo, wamekuwa wakiomba bila kuchoka ili serikali ili wafanye kila njia iwezekanavyo  ili wasicha wawe huru. Lakini Serikali ilitoa jibu kwamba wasingeweza kufanya mkataba, kutokana kwamba ilibidi  kuwaachia huru baadhi ya viongozi wa magaidi wa Boko haram waliokuwa jela. Lakini hatimaye ndicho kitendo kilichotekea.

Kwani ili kuwachia  huru wasichana Serikali imewaachia baadhi ya Viongozi wa Boko Haram na wamelipa kiasi flani kikubwa na muhimu. Je hiyo isingefanyika mapema kuzuia miaka miatatu ya mateso ya hawa wasichana na familia zao? anasema Kardinali... Miaka mitatu ya mateso, ingeweza kuzuiwa,anasisitiza Kardinali Onayeikan,na kwamba haitambuliki ni mateso gani vijana hawa wamepitia, lakini inatosha tu kuwaona nyuso zao katika televisheni kwa kutambua zaidi kipindi kigumu na cha kutisha walichopitia. Aidha anasema, kati yao  kuna msichana ambaye amefika bila kuwa na mguu je ni nani  anaweza kupima na kufidia maafa ya kisaikolojia waliyoyapata?

Kardinali Onayeiyekan anauliza swali tena, je iwapo kati wa  watoto hao angekuwapo  mmojapo wa watu wenye madaraka,je wangepoteza muda wote huo?. Halikadhalika  anabainisha, pamoja na hao kuachiwa huru isisahulike kuwa bado wasichana zaidi ya 100 ambapo haijulikani mwisho wao utakuwaje. Anasema,labda wengine kati yao wamekufa kutokana na mapambano, au magonjwa wakati wa kujifungua watoto,kwani inasadikia kuwa wengi wao wamebeshwa mimba na watekaji nyara.Kardinali kwa masikitiko yake anasema; ingekuwa vema angalau wazazi wao wakapata taarifa juu ya mwisho wa maskini wasichana hawa. Kwa njia hiyo Kardinali anatoa wito kwa watu wot kusali kwa ajili uhuru wa wote waliobaki mikononi mwa watesi wao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.