2017-05-05 16:18:00

Papa: Usiwe mgumu wala kuishi kinafiki inahitajika unyenyekevu!


Hata leo katika Kanisani kuna watu ambao wanatumia ugumu kufunika dhambi zao. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko alio utoa wakati wa mahubiri yake Ijumaa asubuhi tarehe 5 Mei 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Akichambua somo la kwanza kutoka  kitabu cha matendo ya mitume , Baba Mtakatifu amesimama  kutazama sura ya Mtakatifu Paulo, ambaye kwa ugumu wake wa kutesa Kanisa anageuka kuwa mnyenyekevu na mvumilivu wa kutangaza Injili kwa watu wote. Baba Mtakatifu anasema ni kwa mara ya kwanza jina la Sauli linatokea kwasababu wakati  Stefano anauwawa kwa kupigwa mawe,  Sauli alikuwa ni kijana mgumu , mwenye itakadi kali katika ugumu wa kushikiria sheria. Anaongeza, alikuwa mgumu lakini alikuwa  mwaminifu. Yesu alimjia kwasababu alitaka kuhukumu ugumu ambao haukuwa wa kiaminifu.Wapo watu wagumu ambao wanaishi namna mbili ya kinafiki, kwasababu wanajionesha mbele kuwa wazuri,waaminifu, lakini wasipoonwa na mtu wanafanya mambo mabaya.

Lakini kijana huyo alikuwa mwaminifu, yeye alikuwa anaamini kile anachosema . Anatoa mfano kuwa hiyo anawaelezea  vijana mambo haya hasa wale waliojaribiwa na vishawishi vya ugumu katika Kanisa la leo hii. Wengine ni waaminifu na ni wema, lakini inabidi kuwaombea ili Bwana aweze kuwasaidia kukua katika njia ya unyenyekevu. Baba Mtakatifu anaendelea, wengine wanatumia ugumu kufunika udhaifu , dhambi, magonjwa binafsi, na hutumia ugumu kwa ajili ya kusema ya wengine. Aidha anaendela kutazama Paulo  kwa undani ,anasema, Sauli aliyekulia katika mazingira ya ugumu na kwamba, huwezi kukataa kwamba alikulia katika mazingira ya uasi wa Mungu hadi kutesa wakristo. Angalau historia yake  ilikuwa inawaach na butwaa watoto wengi. Lakini leo hii hakuna! Hivyo basi Mtakatifu Paulo wakati yuko njiani Damasko kuwachukua wafungwa wakristo kutoka Yerusalem, ndipo anakutana na mtu mwingine akiongea kwa lugha ya unyenyekevu, ”Sauli, Sauli mbona unanitesa? 

Mtoto alisema kijana mgumu amekuwa mwanaume mgumu, lakini mwaminifu, aligeuka kuwa mtoto na kuacha apelekwe mahali ambapo Bwana alimwita. Hiyo ndiyo nguvu ya unyenyekevu wa Bwana . Ndiyo maana  Sauli aligeuka kuwa Paulo  na kumtangaza Bwana hadi mwisho na kuteseka kwa ajili yake
Mwanaume huyo katika uzoefu wake anatangaza Injili kwa watu wengine, kwa upande mwengine watu wanaoteseka , wenye matatizo , na hata katika kanisa , vilevile hata yeye aliteseka na wakristo wenzake walio kuwa wakigombana kati yao. Lakini yeye pamoja na kwamba alikuwa mtesi wa Bwana kwa ajili ya kushikiria Sheria, baadaye atawaelezea Wakristo kwamba pamoja na jinsi wanavyoishi mbali na Bwana kwasababu ya dhambi katika akili, mwili na vyote kwasasa ni wakamilifu na wampe sifa Mungu.

Kuna mazungumzo ya kutosha kati ya ugumu na unyenyekevu, Baba Mtakatifu anasema , mazungumzo kati ya mtu mwanifu na Yesu anayezungumza naye kwa upole. Ndivyo ilivyo anza safari ya mwanaume huyo tuliye mtambua akiwa kijana , wakati wa kupigwa mawe mtakatifu Stefano, lakini  baadaye naye Paulo  ataishia kusalitiwa na baadhi ya wakristo . Kwa maana hiyo baadhi ya watu wengine watafikiria maisha ya Mtakatifu Paulo yalishindwa kama vile walivyo mfikria hata Yesu. Baba Mtakatifu amemalizia akiwataka wakristo wote kufuata njia ya Yesu aliyotuachia, njia ya kutangaza Injili, njia ya mateso, njia ya msalaba na njia ya ufufuko.  Kwa maombezi ya Sauli kwa namna ya pekee kuwaombea wale wagumu wanaoishi ndani ya Kanisa,ni wagumu lakini waaminifu kwa Bwana,wanampenda Bwana lakini wanakosea. Kwa ajili ya wanafiki wagumu, kwa wale wanaoishi maisha ya kinafiki, ambao Yesu alisema fanyeni yale wasemayo lakini siyo yale wafanyao. Tusali kwa ajili ya wagumu leo hii.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.