Katika kilele cha kuadhimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Kipapa ya Kanisa la Romania mjini Roma , Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanachuo na kutoa hotuba yake tarehe 5 Mei 2017 kwa ajili ya kuwatakia heri. Katika hotuba hiyo anasema, anayo furaha ya kuwasalimia wakati wanafanya kumbukumbu hiyo ambayo ni fursa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu pia wote ambao kwa miaka hii wamejikita katika juhudi zao kwenye Taasisi ya Pio Romeno katika mchango wao wa kutoa mafunzo kwa makleli wa maisha endelevu. Njia yao wanayoifanya ni sehemu inayojikita katika historia iliyoendelea, ambayo ni matokeo ya badaye kwa ajili ya Makanisa ya Kigiriki na wakatoliki wa Romania. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawatakia heri ya mambo mawili kwanza kutunza kumbukumbu na kukuza matumaini.
Katika kufafanua maana ya kutunza kumbukumbu anasema,Taasisi hiyo imetokana na na uwepo wa muda mrefu jumuia ya wakatoliki wa mashariki, na pia kuguswa kwa undani juu ya matukio ya kusikitisha zaidi yanayohusu utesi wa Kanisa ,ambapo kwa miaka ya karibuni wamejifungua zaidi katika kukabiliana na changamoto. Katika historia hiyo imeunda mashahidi wengi wa Imani katika kipindi kigumu cha majaribu, kipindi cha giza na cha mwanga ambapo matukio yote haya yanawagusa ninyi kwa karibu. Kwa njia hiyo ni vema kutunza kumbukumbu, lakini msikubali kukandamizwa na kushikiria nyakati za nyuma ni lazima kuishi matukio katika wakati uliopo.Hiyo ni kwa msaada wa Injili iliyo hai, ambayo inakumbatia historia kubwa zaidi ya maisha yenu, pia jifungue wazi kwake Roho Mtakatifu. Iwe tunu kwenu kwa njia ya sala na masomo ya kina, ambayo Bwana alifunua kazi kubwa kwa njia ya watu wake kwasababu hiyo ni fursa kubwa kwa miaka mnayoishi Roma , maana mnaweza kupunua hali ya umoja wa Kanisa.
Katika kuhimarisha kumbukumbu ya Kanisa , mtasaidiwa kushinda majaribu ya hatari
ambayo yanaweza kuonekana katika mambo yasiyo kuwa na maana hasa katika kufurahia
maisha ya kawaida , mahali ambapo kila kitu kinaelendelea mbele bila kuwa na shahuku
wala harufu hatimaye mnaishia kuwa walezi wenye wivu na wavivu ambao wanashikiria
kulinda usalama na ustawi binafsi.
Kwa njia ya mifano hai ya kuonja zawadi ya injili, kuweni wachungaji ambapo kila
mchungaji anafananishwa na Kristo aliyetoa maisha yake na kuwapenda mpaka mwisho(Yh
13,1). Haiwezekani kabisa kushuka kwa kujikita katika mambo yasiyo stahili na bila
kujihatarisha. Daima Taasisi hiyo iwe kama uwanja wa kafanya mazoezi ya kutoa maisha
katika uwajibikajii wa masomo yenu ambayo ndiyo zana za huduma kwa kanisa. Ni tajiri
kwa ajili ya utamaduni wa nchi yenu, ambao lazima kutunza kumbukumbu, ambayo siyo
tu kufikiria mambo yaliyo pita bali kuishi kwa matumaini.
Baba Mtakatifu anaelezea matashi mema ya pili, maana ya kukuza matumaini kwamba,kuna
haja moja muhimu ya kukuza matumaini ya kikristo , matumaini yanayotoa mtazamo mpya,
wenye uwezo wa kugunduua na kutazama mema, hata mahali ambapo kuna giza la ubaya.
Mtakatifu Ephraimu aliandika kuwa “iwapo matumaini ni hai katika mitazamo yetu, tutaona
yale yaliyojificha”. Hata katika Kitabu cha Matendo ya mitume ambapo Liturgia ya Pasaka
inatushauri,inaonesha jinsi gani Kanisa linaishi katika matumaini ya mfufuka, kuishi
katika sala, umoja na upendo .Haupotezi kamwe mtazamo na kutoa matumaini hata mahali
ambapo hawaeleweki na bila kuwa na zana za kuwasadia. Roho Mtakatifu aongeze ndani
yao shuhuku ya kutafuta na kuhamasika kwa moyo wote njia ya mapatano na umoja kati
ya wakristo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |