Bwana ilainishe mioyo migumu, ambayo uhukumu kila kitu kilicho kinyume na sheria. Hayo ni maombi ya Baba Mtakatifu Francisko katika Misa ya asubuhi Jumanne tarehe 2 Mei 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican. Hawatambui ya kwamba huruma ya Mungu ina uwezo wa kugezua mioyo migumu kama mawe na kuwa ya nyama. Mtakatifu Stefano ni shahidi wa utii, kama Yesu na ndiyo maana aliteswa. Baba Mtakatifu akitafakari somo la siku juu ya kifodini cha Mtakatifu Stefano, anasema, mkristo ni shahidi wa utii. Waliomtupia mawe Stefano hawakuwa na utambuzi wa Neno la Mungu, na ndiyo maana Mtakatifu Stefano aliwaita wenye shingo ngumu , wasio tahiriwa katika mioyo na katika masikio . Baba Mtakatifu anafafanua, mtu ambaye hakutahiriwa kwa nykati hizo ilikuwa sawasawa na mpagani.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaomba kutafakari namna ya kuwa na utambuzi wa Neno
la Mungu katika Injili ya siku. Anasema Kwa mfano wa Yesu aliwaita mitume wa Emau
wapumbavu , hayo ni maelezo yasiyo toa sifa japokuwa hayana nguvu kama yale aliyotumia
Stefano.
Mitume wa Emau hawakujua, kwasababu walikuwa na hofu, hiyo ni kwasababu hawakutaka
kujiingiza katika matatizo, ilikuwa ni hofu tu japokuwa wao walikuwa ni wema na wako
wazi katika ukweli. Wakati Yesu anawakaripia akifafanua maandiko matakatifu waliacha
maneno yake yaingie ndani yao na mioyo yao ikawaka tofauti na na wale walio mtupia
mawe Stefano , walikuwa na hasira kuu, hawakutaka kusikiliza. Baba Mtakatifu anasema
hili ni janga la kufunga mioyo na kuwa migumu.
Zaburi ya 94 inawashauri watu wake wasifanye mioyo yao kuwa migumu. Hata Nabii Ezekieli anafanya ahadi nzuri ile ya kubadili mioyo migumu kama mawe kuwa nyama, maana yake moyo wenye uwezo wa kusikiliza na kupokea ushuhuda wa utii. Mioyo migumu kama mawe inafanya Kanisa liteseka sana Baba Mtakatifu anasema hayo kwa uchungu,mioyo ambayo haitaki kufunguka na wala kusikiliza. Mioyo ambayo siyo kwa kutambua tu lugha ya kuhukumu bali inatambua kuhumu hasa, haiwezi kusema, bali inauliza kwanini unasema hivi, kwanini hiki, nieleze…ni mioyo iliyofungwa , wanajifanya kuelewa kila kitu na kwamba hawana haja ya kuelezea.
Kitendo cha Yesu kuwakaripia waliowaua manabii , ilitokana na kwamba waliwaelezea mambo ambayo hakuwa wanapenda . Hayo yote ni kwasababu moyo ulio fungwa hatuoi nafasi ya roho mtakatifu aingie. Hapakuwapo na nafasi ya Roho Mtakatifu katika mioyo yao. Lakini katika somo linaeleza kwamba Mtakatifu Sefano akiwa amejaa Roho Mtakatifu alikuwa ametambaua yote. Yeye alikuwa ni shuhuda wa utii wa Mungu ambaye ni Neno aliyefanyika mwili. Kwa njia hiyo, moyo uliofungwa, mgumu , moyo wa kipagani hawezi kuacha nafasi ya Roho mtakatifu aingie kwa sababu ya kujitosheleza.
Baba Mtakatifu Francisko anasema mitume wawili wa Emau ndiyo sisi, pamoja na wasiwasi
, dhambi ambazo mara nyingi tunatamani kwenda mbali na masalaba , na majaribu. Ni
bora kuacha nafasi , ili mioyo hiyo iwashwe na Yesu mwenyewe.
Aidha Baba Mtakatifu Francisko amelezea juu ya watu wale ambao walikuwa wagumuna mioyo
yao imefungwa kwa kushiria sheria, na hawakutaka kusikiliza Yesu… wao walikuwa wanaongea
mambo mabaya zaidi ya yale yaliyo tamkwa na Mtakatifu Stefano. Baba Mtakatifu anaoanisha
kitendo cha mawe na mfano wa mwanamke mzinzi, kwamba kila mmoja aweze kuingia katika
mazungumzo kati ya moyo mgumu na Yesu, ambapo moyo mguni ni kama wa yule mwathirika
mwanamkwa ambaye Yesu aliwajibu wale waliokuwa wakitaka kumtupia mawe ya kwamba watazame
ndani ya mioyo yao.
Kwa kumalizia Baba Mtakatifu amesema ni kutazama huruma ya Yesu, Shahidi wa uti, ambaye ni shahidi mkubwa aliye toa maisha kwa kutufanya tuonje huruma ya Mungu sisi wenye dhambi na wadhaifu. Pia tuweze kuingia katika mazungumzo na kuomba neema ya Bwana alainishe kidogo mioyo yetu migumu, hata kwa wale wenye mioyo iliyofungwa daima katika kushikiria sheria wakihukumu kila kitu kitu kilicho kinyume na sheria yao. Kwasababu hao hawajuhi kwamba Neno alifanyika mwili na kwamba Neno ni shahidi wa utiii. Hawajui kwamba huruma ya Mungu inao uwezo wa kubadilisha mioyo migumu kama mawe na kuwa mioyo ya nyama.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |