2017-05-01 15:06:00

Tuombe mani na mapatano katika nchi ya Venezuela na Macedonia!


Kuna habari za kusikitisha zinazo vuma kutika dunia kwa namna ya pekee kutoka nchi ya Venezuela. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa mbingu  na baada ya hotuba yake katika Mkutano na wanachama  wa chama Katoliki cha Vijana Jumapili 30 Aprili 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Petro.Baba Mtakatifu amesema ni taarifa za kusikitisha juu ya hali mbaya ya Venezuela  kutokana na kuongezeka machafuko   na idadi ya vifo, majeruhi na kutiwa mbaroni  watu wengi ndani ya nchi. Anasema, “wakati nashiriki mateso ya familia zilizo athirika kwa sala, ninarudia wito  viongozi wa Serikali ya nchi pamoja na wapinzani ili kuweza  kusitisha aina zozote za vurugu  na kupata muafaka  wa kuheshimu haki zote za kibinadamu na kutafuta ufumbuzi, katika mchakato wa kuondoa kipeo  cha kutisha cha kibinadamu, kijamiii, kisiasa na kuichumi kinachoikumba idadi kubwa ya watu.

Baba Mtakatifu Francisko amewakabidhi kwake  Bikira Maria  katika maombi ya amani,mapatano na demokrasia ya nchi hiyo na hata kuomba kwa kwa ajili ya nchi nyingine zinazopitia kipindi kigumu kama vile nchi ya Jamuhuri ya Masedonia. Aidha amekumbuka Mwenye heri mpya wa Kanisa Leopoldina Naudet, Mwanzilishi wa Shirika la Familia Takatifu aliyetangazwa kuwa mwenye heri Jumamaosi 29 Aprili 2017 huko Verona nchini Italia wakati huo pia amekumbuka Siku ya maadhimisho ya Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu wa Yesu Milano,maadhimisho yaliyofanyika tarehe 30 Aprili 2017 ,anawatia moyo kuendeleza  taasisi hiyo muhimu na kuendelea kujikita katika kuwekeza juu ya mafunzo ya vijana ili dunia iwee kuwa bora.

Pamoja na siku hiyo, pia  Baba Mtakatifu ametoa shukrani zake kwa ajili ya mpango wa Jumapili ya Biblia , iliyo andaliwa huko nchini Poland katika makanisa, mashule , na katika mitandao ya kijamii ili kusoma maandiko matakatifu. Mwisho anashukuru Maria Mama yetu kwa ajili ya ulinzi wake kufanikisha ziara yake ya kitume nchini Misri iliyo malizika Jumamosi  29 Aprili 2017. Ameomba Bwana awabariki watu wote wa Misri kwa ajili ya ukarimu wao na makaribisho aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa nchi, waamini wakristo, waislam na Mungu awape amani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.