2017-05-01 15:24:00

Kuombea Bara la Afrika katika nia ya maombi ya mwezi wa Tano 2017!


Katika nia za jumla za Baba Mtakatifu Francisko kwa  mwezi wa Mei,  2017, ni kwa ajili ya Wakristo Barani Afrika ili waweze kuiga mfano wa Yesu Kristo mwingi wa huruma, ili kweli waweze kuwa ni mashuhuda na vyombo vya haki, amani na upatanisho! Waoneshe ushuhuda wa kinabii katik maisha yao ya kila siku. Nia hizi za Baba Mtakatifu zinasambazwa kwenye mitandao kwa njia ya Utume wa Sala Kimataifa. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.