2017-04-30 15:34:00

Kard Bagnasco:Miaka 150 ni fursa ya kumbukumbu ya kihistoria !


Tarehe 27 Aprili 2017 Chama cha Kitume cha Vijana Katoliki kimeadhimisha Jubilei ya miaka 150 tangu kuanzishwa kwake kwa ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko kikamilifu. Maadhimisho haya yamewashirikisha hata wajumbe wa Kimataifa kutoka sehemu mbali mbali za dunia kuanzia tarehe 27-30 Aprili 2017 ambapo kwa pamoja wanachama wamekusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro katikakushiriki sala ya Malkia wa Mbingu kwa kuwa bado ni kipindi cha Pasaka . Maadhimisho ya Jubilei ya miaka 150 ya Chama cha Kitume cha Vijana Wakatoliki Italia imeongozwa na kauli mbiu “ Utume wa Vijana Wakatoliki kwa ajili ya pamoja na wote”. Mandalizi ya jubilei kufanyika mjini Vatican  yamefanywa na Shirikisho la Vyama vya Utume wa Vijana Kimataifa (FIAC), wakati wanajumbe 50 kutoka kila nchi wanachama na watazamamaji  40 wameshiriki  kuwachagua viongozi wapya katika mkutano wa kumi na sita.

Wajumbe wengi kutoka kila jimbo nchini Italia wameshiriki katika makutano kwa siku hizo ambapo wamechagua wajumbe wa kuunda  viongozi wao kuitaifa. Huo umekuwa mwafaka wa maisha ya utume wa Kanisa kwa vijana wakati Kanisa linapofanya maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana, ambayo itakwenda sambamba na siku ya 34 ya Vijana Duniani  huko Panama.
Katika kuadhimisha Jubilei ya miaka 150, hata Baraza la Maaskofu nchini Italia wametoa ujumbe wa, kuwatakia heri na ufanisi wa maisha ya kitume ya vijana katika Kanisa. Ujumbe ulio tiwa sahini na Kardinali Angelo Bagnasco Rais wa Baraza la Maaskofu Italia unasema; Maadhimisho ya miaka 150 ya kuanzishwa kwa Chama hiki hawali ya yote ni fursa ya Kanisa la Italia kutoa asante kwa uwepo wao,asante kwa uaminifu wao kwa Kanisa lilipowaomba kufikiria na kufanya mabadiliko ya muundo, mbinu na lugha ya kutumia.

Asante kwa juhudi zao kwa ngazi ya watu,katika ukomavu na uchaguzi unao ofanywa na kila  jimbo katika utekelezaji kwa njia ya  miongozo ya mitaguso ya Kanisa, katekesi, liturugia, ushuhuda wa upendo, hata namna ya miundo mbinu ambayo ndiyo tabia ya Kanisa katika umoja na kujikita katika kutoa huduma ya  umisionari.Asante kwa uthibitisho wa kuchagua dini kwa maana ya mafunzo ya kilei ili kuweza kukabiliana na changamoto za kizamani, na kisiasa katika kutoa ushuhuda wa thamani ya kikristo; Asante ninyi kuwa shule ya utakatifu, hiyo ni kutokana mifano mingi za utakatifu wa walei ambao wametambuliwa na Kanisa na wengine wasio julikana lakini Mungu peke yake ajua matendo yao, japokuwa kwa upande mmoja uwepo wenu ni ishara yao, kwa upande mwingine ninyi ni kama dhahabu inayo endelea kufanya sehemu mojawapo ya uwajibikaji mpya ndani ya Kanisa.

Kuadhimisha miaka 150 ni fursa ya kufanya kumbukumbu ya historia ndefu, ya matukio mengi, mabadiliko, uchaguzi wa kijasiri uliofanyika na hata bila mafanikio na zaidi sura nyingi zilizo jikita kwa ujasiri kufanya uzoefu wa aina yake ya kihistoria ambayo siyo kwa Kanisa tu bali hata katika Taifa zima. Lakini ili kuepuka  majuto ya siku za nyuma, maadhimisho haya yawe fursa muhimu kujikita  upya katika shughuli za  kilei  katika kutoa huduma ya kujitolea  katika Kanisa na ulimwengu. Ujumbe unakumbusha Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko alipotembelea Firenze yasemayo kuwa  “Leo hatuwezi kuishi enzi ya mabadiliko na mabadiliko ya enzi. Hali tunayoishi leo inakabiliwa na changamoto mpya na wakati mwingine ni vigumu kuelewa. Katika nyakati  hizi tunalazimika kuishi na matatizo kama na isionekane kama vikwazo, kwasababu Bwana anafanya kazi ya duniani.”Kwa maana  hiyo enendeni babarani mkawaite wote bila ubaguzi”. (Taz Mt 22,9).

Ili kuelewa hili, jambo muhimu ni lazima kutangazwa na kusambazwa lakini kwa uchaguzi na ubunifu, kwa kutumia lugha mpya ,kufanya mafunzo  ili kutambua vema  na kutoa mapendekezo muhimu kwamba lazima kuishi ndani ya Jumuia za kanisa na katika jamii kwa kuanzia katika chama katoliki cha vijana wenyewe.Mang’mauzi ya dhati ndiyo mchakato wa kuwafikisha kutambua mema ili kupata kuwaongoza kushiriki kikamilifu  na siyo kutafuta utulivu wa tabia ya maisha, wala kuwa watazamaji bali kuwa kuwajibika kwa ajili ya faida ya wote kwa kuamua  nini cha kufanya  na sasa kwa hiari bila kukumbushwa.Katika ibara ya katiba (art.13.2) ya  Chama Katoliki cha Vijana, tayari inaonesha umuhimu wa kufanya mafunzo kwa sababu Injili ndiyo ndiyo ina uwezo wa kuongoza maisha. Hiyo inahusu kuwa wazi zaidi na uhalisia wa malengo na mipango ya mafunzo.Kufanya hivyo ni kweza kugundua kwa upya umuhimu wa ubatizo na pia kwamba ni matunda ya wito na zawadi asili ya kiroho ambayo binadamu amepokea.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.