2017-04-30 15:06:00

Historia nzuri ya maisha ni kuwa na macho yanayo tazama nyuma!


Katika kilele cha kuadhimisha miaka 150 ya Chama Katoliki cha Vijana, Baba Mtakatifu Francisko ametoa hotuba yake Jumapili 30 Aprili 2017, kuonesha furaha ya kuwa pamoja nao wakiwa wengi kusheherekea jubilei ya kuanzishwa kwa chama chao. Amewashukuru pia wote kwa hotuba yao waliyo itoa wakati wa kuanza maadhimisho hayo katika viwanja vya matakatifu Petro Vatican. Baba Mtakatifu amesema,kuzaliwa kwa Chama Katoliki cha Vijana ilikuwa ni ndoto iliyotokana na vijana wawili Mario Fani na Giovanni Acquaderni, ambapo baadaye ikawa safari ya imani kwa vizazi vingi,kama vile utume wa afya,watu wengi kuanzia watoto,vijana na hata watu wazima ambao wamekuwa mitume wa Yesu.

Kwa namna hiyo watu hao walionja kuishi kama mashuhuda wa furaha ya upendo na katika ulimwengu. Baba Mtakatifu Francisko ametoa ushuhuda binafsi wa maisha yake  ya kwamba hata katika familia yake , baba namama yake walikuwa wanachama Katoliki cha Vijana. Ni historia nzuri na muhimu, kwa njia hiyo mnayo sababu ya kutoa shukrani kwa Bwana ambapo pia Kanisa lina utambuzi huo. Ni historia iliyo undwa na watu wa kila rika na hali, ambao wamekuwa na shahuku ya kushi pamoja na kukutana Bwana, wadogo kwa wakubwa, wakiwa na wachungaji pamoja, kila mmoja katika nafasi yake kijamii katika kuandaa utamaduni kila mahali wanapotokea.

Waamini walei  wa nyakati zote  kwa miaka 150,wameshirikiana kutafuta njia bila kuchoka kutangaza uzuri wa maisha yao vilevile ya upendo wa Mungu kwa kushirikiana katika kujikita zaidi kwenye ujenzi wa jamiii ya haki, undugu na mshikamano. Ni historia ya upendo mkubwa kwa ulimwengu na Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko amekubusha kitabu kilicho andikwa  huko Argentina mwaka 1937  kuhusu “ Chama Katoliki cha Vijana na upendo katoliki “ ya kwamba ni historia iliyo ndani ambayo inaonesha sura inayo ng’aa ya wanaume na wanawake wa imani ya kuigwa, ambao wamehudumia nchi kwa ukarimu na ujasiri.

Lakini Baba Mtakatifu Francisko anafafanua zaidi akisema, kuwa na historia nzuri siyo lazima,bali kutembea katika njia kwa macho yanayo tazama nyuma,: kwa mfano hakuna ulazima wa kujitazama katika kioo, wala kukaa vema katika sofa!  usijitazame katika kioo!; kwa kutania Baba Mtakatifu amesema “kwasababu wengi tu wabaya na hivyo bora usijitazame”!, ameendelea “usikae  katika sofa kwasababu utanenepa na kuugua magonjwa ya mafuta!: kwa kufafanua zaidi juu ya hilo “ Jambo muhimu ni kufanya kumbukumbu ya safari ndefu ya maisha ambayo inasaidia  kujitambua kuwa binadamu anaye saidia wengine,kila mmoja katika kukua kibinadamu, katika imani kwa kushirikishana huruma ya Bwana anayozidi kuitoa kwa ukarimu wake. 

Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo kuendelea kuwa mitume wa kimisionari ambao wanaishi na kutoa ushuhuda wa furaha, wakitambua kwamba Bwana anawapenda kwa upendo upeo, na pia kupenda  historia kwa pamoja ambamo wanaishi.Kwani hayo ndiyo mafundisho ya mashidi watakatifu ambao walipitia katika njia ya Chama Katoliki cha Vijana. Aidha amependa kuwakumbuka waamini hao kama vile; Toniolo, Armida Barelli, Piergiorgio Frassati, Antonietta Meo, Teresio Olivelli, Vittorio Bachelet. Na kuogeza kusema kuwa “Chama Katoliki ishini kadiri ya historia yake! Ishi kadiri ya wanaume na wanawakae  hawa waliotangulia!.

Kwa miaka 150 Chama Katoliki cha Vijana daima kimekuwa na tabia ya upendo mkubwa wa Yesu na kwa Kanisa. Hata leo mnalikwa kufuata wito huo katika kujikita kwenye huduma ya Jimbo kwa maongozi daima ya  Askofu,na kuishi katika parokia ambamo Kanisa linaishi ndani ya maisha ya kila mmoja. Watu wote wanafaidika na  matunda ya utume wenu  ya kuishi kwa umoja kati ya Kanisa mahalia na ulimwengu. Ni katika wito wa kilei na utakatifu wanaoishi kila siku,ambao mnaweza kupata nguvu na ujasiri wa kushi wa imani ,mkibaki mahali mlipo kwa kukaribisha, kufanya mazungumzo ; namna ya kuwa karibu na wengine, kufanya uzoefu wa uzuri wa kushirikisha na uwajibikaji. Baba Mtakatifu Francisko amesema, msichoke kutembea katika barabara ambazo inawezekana kukuza mshikamano wa dhati kwa watu wa Mungu. Na kila mmoja anaweza kuchangia katika kutambua  kwa makini ishara za nyakati, kwa njia ya  sala za mara kwa mara na  kuelewa kuishi mapenzi ya Mungu mkiwa na uhakika ya kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi na kufanya mambo yote kuwa mapya kila siku.

Baba Mtakatifu Francisko amewaalika kupeleka mbele uzoefu wa kitume ambao umetanda mizizi katika parokia kwani amasema, Parokia “siyo muundo ulio haribika”; amesisitiza kama wameelewa; Parokia siyo muundo ilio haribika; kwasababu uwepo wa Kanisa katika maeneo ni kusikiliza Neno, kukua katika maisha ya kikristo, mazungumzo, kutangaza, kufanya matendo ya upendo, kuabudu na kuadhimisha ibada (Taz:Furaha ya Injili 28). Parokia ni nafasi ambayo watu wanaweza kujisikia kupokelewa jinsi walivyo, wanaweza kusindikizwa katika njia ili kufikia kukomaa kiutu na kiroho, kukua katika imani na upendo, kwa viumbe na ndugu. Lakini kukomaa huko inawezakana tu iwapo Parokia haitajifunga yenyewe binafsi, iwapo hata Chama Katoliki kinachoishi ndani ya parokia akijifungi binafsi badala yake kiko wazi kinasaidia Parokia kubaki katika mawasiliano na familia, na katika maisha ya watu. Muundo wa Parokia usigeuke uliotengana na watu au kikundi cha wasio amini kutazamana  wao binafsi.

Baba Mtakatifu amerudia kusema hiyo tafadhali isifanyike! Badala yake kila aina ya mpango, kila aina ya mapendekezo na kila aina ya uzoefu wa kimisionari kwa mantiki ya kuinjilisha, isijisikie  kujitosheleza badala yake, kutokana na kuwa sehemu katika parokia wajikite katika safari kwenda  pembezoni, kwenye mitaa ya miji, wilaya na miji. Kwa jinsi ilivyojitokeza miaka hii ya mia moja hamsini , wajisikie ndani yao nguvu ya uwajibikaji na kupanda mbegu njema ya Injili katika maisha ya ulimwengu, kwa njia ya huduma ya upendo, katika majukumu ya kisiasa na wajikite ndani ya siasa lakini katika siasa kubwa  kwa maana ya siasa ya elufi kubwa, kuwa na shauku ya elimu na kushiriki katika mambo ya utamaduni.
 Panueni mioyo yenu kwa ajili ya kupanua mioyo ya parokia. Jikiteni katika safari ya imani kwa ajili ya kukutana na wengine, kuwapokea, kuwasikiliza na kuwakumbatia wote. Kila maisha yanayo mpendeza Bwana na kila uso wa mtu ni uso wa Kristo, hasa wale maskini, walio jeruhiwa katika maisha yao, wale wanao hisi kutelekezwa, wale wanao kimbia kifo na kutafuta ulinzi katika nyumba zetu na katika miji yetu. Kwasababu  “hakuna mtu anaye samehewa kutokana na wasiwasi juu ya maskini na wanao tafuta haki za  kijamii” 

Mbaki wazi katika hali halisi inayo wazunguka, kutafuta kuzungumza bila hofu na wale ambao mnaishi nao karibu, hata  wale wanao wafikiria kinyume na jinsi mlivyo katika wenye kutamani amani, haki na undugu. Ni kwa njia ya mazungumzo yaweza kuwafanya kuwa wabunifu wa mipango ya pamoja ya baadaye. Ni kupitia mazungumzo ambayo tunaweza kujenga amani kwa wote na kuzungunza na wote. Baba Mtakatifu Francisko amemalizia hotuba yake akiwatakia wanachama wote wadogo kwa wakubwa kwenda pembezoni ambapo amesema, pale wawe Kanisa kwa nguvu za Roho Mtakatifu na  kwa njia ya ulinzi wa Bikira Maria mkingiwa wa dhambi ya asili.Na pia kwa njia ya kusindikizwa na kutiwa moyo wa maaskofu wao mahalia.

Na Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.