2017-04-29 16:28:00

WCC:kushirikisha imani kwa vizazi endelevu uwajibu wa Kanisa!


Nini maana ya nafasi ya Makanisa katika ujenzi wa amani, je ni changamoto gani na fursa zipi za kiekuene zinazojitokeza? Ni baadhi ya maswali ya kujiuliza katika meza ya mduara wa kikundi cha kazi wa  Baraza la Makanisa Ulimwenguni (World Council of Churches - WCC) na Kanisa Katoliki walio kutana kuanzia tarehe 24- 26 Aprili 2017 mjini Dublin Ireland. Mwaliko wa mkutano huo ulitolewa na  Askofu Mkuu wa Dublin Diarmuid Martin ambaye pia alikuwa mmoja wa wasimamizi wa kikundi cha kazi pamoja na Askofu Mkuu Nifon  wa Targoviste.

Katika mkutano huo pia uliudhuriwa na mwakilishi wa Baraza la Kipapa  kwa Kuhamasisha Umoja wa Kikristo, Katibu Askofu Brian Farrell na Andrzej Choromanski muhusika wa mahusiano ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc).Katika hotuba yake,Monsinyo Martin amesisitiza umuhimu wa kushirikishana  imani kwa vizazi endelevu na wajibu wa Kanisa kuhusu jumuya  za wahamiaji. 

Nafasi kubwa ya mazungumzo katika meza ya mduara  ilikuwa ni kutazama  kwa upya mafanikio yaliyo patikana katika Makanisa kuhusiana na suala la uhamiaji na ujenzi wa amani. Kwa mtazamo huo wamesema kuwa, kuna ulazima wa kutoa jibu kama wakristo  dhidi ya majanga makubwa yanayo wakabili watu hasa kulazimika kuhama katika hali ngumu sana.

Na Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.