2017-04-28 15:15:00

Zambia:Maaskofu wanalaani vitendo vya polisi kutumia nguvu!


Haiwezekani polisi kujihusisha na mambo ya kisiasa. Ni onyo kutoka  katika Baraza la Maaskofu wa Zambia , mara baada ya kukamatwa  kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema katika hali isiyo ya kawaida. Kiogozi huyo ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kusaliti, kwamba ndiye aliyesababisa kuweka kuzuizi cha msafara wa magari ya Rais Edigar Lungu maghaharibi mwa nchi. Ilkuwa tarehe 11 Aprili 2017 polisi nchini Zambia walimtia mbaroni Hakainde Hichilema ambaye ndiye kinara wa chama kikuu cha upinzani cha United Party for National Development. Maafisa wa polisi walivamia wakati wa usiku na kubomoa milango ya  makazi ya Hichilema na kumtia mbaroni bila kutoa maelezo yoyote kwa familia yake, na wala waranti pia kurusha mabomu ya kutoa machozi.

Katika ujumbe wa Baraza la Maaskofu ulio tiwa sahini na Rais wa Baraza hilo Askofu Mkuu Telephore George Mpundu wa Jimbo Kuu Lusaka unasema , wanakosoa na kupinga vikali hatua ya kutumia nguvu iliyo fanyika kumtia mbaroni kiongozi huyo, je pasinge tumika  njia nyingine ya kizalendo na kitaalam kumwita katika ofisi ya mkuu wa Polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka anayotohumiwa?
”Tunalaani tabia mbaya ambapo makundi mara moja yakishika hatamu ya madaraka hutumia polisi kutatua matatizo yao binafsi, kisiasa na kuzuia wapinzani wao kujipanga kufanya kampeni yao ya kisiasa, na kutaka kuwa na mitazamo yao wenyewe juu ya nchi. Imekuwa siku zote hadithi inayofanana kutoka utawala mmoja hadi mwingine, na hiyo haina ubaguzi”. Hivyo maaskofu wanamalizia wakisema, ”waache nchi iweze kujikimu kuliko kuishia katika hila za kisiasa na rushwa”.

Ikumbukwe kuwa  Oktoba mwaka jana, polisi ya Zambia iliwatia mbaroni Hichilema na Geoffrey Mwamba, Mkuu na Naibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha United Party for National Development kwa tuhuma za uchochezi.Uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Agosti mwaka jana huko Zambia ulikuwa wenye ushindani mkali kati ya Rais wa sasa wa nchi hiyo Edgar Lungu na mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema ambaye alidai kuibiwa kura.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.