2017-04-27 17:27:00

Askofu mkuu D'Errico ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Malta


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Alesandro D’Errico kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malta. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Alesandro D’Errico alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Croatia! Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Alesandro D’Errico alizaliwa tarehe 18 Novemba 1950 huko Frattamaggiore, Jimboni Aversa, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 24 Machi 1974 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Kunako tarehe 14 Novemba 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kumweka wakfu wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Tokeo la Bwana, tarehe 6 Januari 1999. Tarehe 14 Novemba 1998 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Pakistan. Tarehe 21 Novemba, 2005, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bosnia-Erzegovina. Tarehe 17 Februari 2010 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Montenegro. Tarehe 21 Mei 2012, Papa Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Croatia! Na tarehe 27 Aprili 2017, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malta.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.