Inabidi kupinga vizuizi vinavyozuia kukaribisha, ndiyo nia kubwa ya ujumbe wa Baraza la maaskofu wa Argentina wakipinga wazo la kubadilisha sheria iliyotolewa katika nchi yao kuhusu wahamiaji. Maaskofu wa Argentina wamesema kwamba hakuna ruhusa katika hali yoyote kwenye ibara ya 8 ya katiba ya nchi hiyo inayokataa au kuzuia haki ya afya, huduma za kijamii au hutoaji wa huduma ya afya kwa wageni wote wanaohitaji msaada na bila kujali hali zao za wanaohama. Ujumbe huo wa Maaskofu uliotolewa hivi karibuni katika vyombo vya habari unasema; nchi ya Argentina daima imekaribisha ndugu na watoto wa wahamiaji kutoka pande zote za dunia na zaidi katika miaka ya hivi karibuni, wahamiaji kutoka nchi zinazopaka na Amerika ya kusini.
Maaskofu hao wamesema ni lazima kuendelea kukuza maendeleo ya utamaduni wa heshima,
mshikamano, na utambulisho kwa Kanisa Katoliki ambao ndiyo unatoa utaofauti kwani.
Hiyo ni kwasababu utambulisho na kupokea ndiyo karama za Kanisa kwa ajili kuwatambua
maskini, waliotengwa katika jamii na wakati mwingine wageni ndiyo wanatuhumiwa kuhusika
na majukumu ya maovu katika jamii ya Agentina.
Kwa mtazamo huo Maaskofu wa Argentina wamesema hakuna haja ya kufanya mabadiliko
ya sheria ya 25871, wakikumbuka ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya Wahamiaji
duniani kwa mwaka 2016 usemao Kanisa linaambatana na wale wote wanaojikita katika
jitihada zao kulinda na kutetea haki ya kila mtu ili aweze kuishi kwa adhi ya kiutu.
Na Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |