2017-04-26 16:21:00

Patriaki Bartholomew kutembelea Jumuiya ya kiekumene Taize Ufaransa


Kwa mara ya kwanza Patriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli ametembelea jumuiya ya Kiekumeni ya Taize nchini Ufaransa .Katika hotuba yake Patriaki Bartholomew amesema; uhusino wa wa Jumuiya ya  Taize na Patriaki wa kiekumene, umeanzia mbali. Ilikuwa mwaka 1962 ambapo ndugu Roger mwanzilishi wa Jumuyia hiyo alifanya ziara ya kiekumene katika Upatriaki wa Atenagora  huko Costatinopoli. Na tangu wakati huo ndugu Roger anakawa rafiki na kuwa na moyo wa kiorthodox  ambao ndiyo utume  na karama ya Jumuiya ya Taize.
Pia unatambua ya kwamba jumuiya yao inatunza na kuheshimu picha ya mama Maria, mama wa mungu ambayo ni kuonesha roho moja ya kindugu katika namna ya kutafuta kukua kiroho chini ya kivuli chake na ulinzi wa mama yetu Bikira Maria; zaidi amesema anajumuisha wote katika mtazamo wa sala zao kama msaada wa wakristo.

Halikadhalika Patriaki Bartholomew amasema, kwa kuonesha  uhusiano kati ya Jumuiya ya Taize na ya Kiorthodox , tarehe 15 Aprili 1963 Kwenye makao makuu ya  Taize walibariki jiwe la kwanza la kiorthodox kuonesha ishara ya uwepo wa jumuia yao usio sahaulika  wa ukristo wa nchi za Mashariki katika kuta za Kanisa hilo; hivyo ni kuonesha leo uwazi wa Kanisa zuri la mapatano.Mada ya mapatano  ni msingi wa ukristo wa binadamu wa Mungu. Kazi ya Kristo katika ulimwengu ni katafuta mapatano ambayo yanakwenda zaidi ya upeo wa dini kwani mapatano yana unganisha kutoka juu kwa muumbaji na kumfikia aliye umbwa yaani binadamu.Mpatano katika Kristo ndiyo kiini msingi ya kumfanya binadamu awe mfano wake Mungu na pia ili aendelee kuwa na mahusiano zaidi ya kufanana yatokanayo na Kristo aliye mpatanishi.

Ngazi ya pili ya inatokana moja kwa moja na fumbo la umoja ambao ni zaidi ya uekumene. Hiyo ni kujibu uwajibu wa kila mkristo  katika kijikita au ulazima katika shughuli za matapano. Aidha ametoa mfanao akisema,kwa  kuonesha picha yake  tunaweza kutumia ile ya uponyaji. Mapatano maana yake zaidi ni kupona majeraha ya kihistoria, yale makovu ya wakati uliopita. Ni kutambuana sisi kwa sisi mafarakano ya zamani na mauaji ya kikatili yaliyofayika  wakati ule. Kwa maana nyingine mgawanyiko wa kikristo uliojitokeza  na ambao sasa tunahitaji kusali kwa ajili ya umoja wa Kanisa umetokana na majareraha ya kiroho ambayo wote tunawajibika; tumeutambua na hata kama hatukubaliani nayo.Kwa sababu hiyo ndiyo  njia ya kiekumene, kwasababu njia ya kiekumene ni kutafuta umoja,kwa kutambua kwamba siyo rahisi kuwapo mapatano  bila kuwa na msamaha.

Ngazi ya tatu ni ile ya ujumla ambayo ni upendo wa Kristo, kwani upendo wa Kristo ndiyo unao tusukuma kufanya mapatano na kuweza kukumbatia binadamu wote. Mapatano yamekuwa ni mada nyeti  kwa ajili kutafuta  amani ambayo imekuwa kwa miaka mingi mazungumzo na changamoto ya kimataifa kwa ajili ya makanisa yetu na dunia kwa ujumla.

Na Sr.Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.