2017-04-26 14:33:00

A.Riccardi na A.Merkel kutafuta njia za mshikamano thabiti!


Bw.Andrea Raiccardi Rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio amepata kuzungumza kwa kirefu na Angel Merkel kabla ya  Mkutano  kuhusu mada ya  maendeleo endelevu ya Ulaya kuanzia vijana na ujenzi wa Amani. Mkutano huo siyo wa mara ya kwanza Ricardi kukutana na Angel; walikutana miaka mitatu iliyopita katika mji Mkuu wa Ujermani, hata katika matukio mengine ya mwezi wa pili 2015, ambapo Kansela wa Ujermani alitembelea  Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Trastevere Roma. Mazungumzo yao zaidi ya dakika 50 yametoa fursa ya kutazama kwa pamoja mada nyeti inayoikabili bara la Ulaya kwa kutazama na kutafuta pamoja mikakati nambinu mpya ya kukabiliana na changamoto. Zaidi ya hayo  mazungumzo yao yamehusu thamani ya ulaya, kwamba siyo kukaa na kubaki wanaangalia na kufikiria nyakati zilizopita bali zaidi hasa ni kuhamasisha  ari endelevu. Kwa njia hiyo ni kutazama mipango ya kushirikishana ambayo ni lazima kuwahusisha hasa vijana wa kizazi kipya. 

Viongozi hawa wamekubaliana wote watatu, Bi Angel Merkel ,Bw.Riccardi na Mkuu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Bw.Marco Pagliazzo aliyeshiriki katika mazungumzo hayo , umuhimu wa kutavumbua ushirikiano wa ajira ambayo itasaidia kuhamasisha thamani ya kijamii na  katika kuongeza mafunzo yanayo saidia vijana kuingia katika  mashindano ya ajira. Katika kuwezesha suala hilo wamesema, inahitaji kurahisisha njia mbadala ili kuzuia ukiritimba unao sababisha daima vizingiti.Aidha katika mazungumzo hayo  Bw.Riccardi na Bw. Marco wamegusia masuala makuu ya matukio ya wahamiaji wakisema, yanapaswa kukabiliwa kwa njia ya kiasiasa pamoja na nguvu za kibinadamu na usalama. Kutokana na mada hiyo, Bi.Merkel ametoa shukrani kwa juhudi zao wanazoonesha  katika mpango wa Njia za Kibinadamu.Ni  mpango ambao Jumuiya hiyo kwa kushirkiana na makanisa ya kiinjili wako mstari wa mbele kujikita katika kuokoa maisha ya wakimbizi na wahamiaji. Njia hizo zimewawezesha kufika nchini Italia hadi sasa wakimbizi 800 kutoka nchi ya Siria kwa Usalama, kwasababu wanasafiri kwa ndege badala ya mitumbwi baharini . Huu ni mfano wa kuigwa katika nchi za Ulaya ambao hata mwezi uliopita, Nchi ya Ufaransa imenzisha.

Halikadhalika kutokana na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kujikita katika  maridhiano na ujenzi wa amani kwenye kanda nyingi za dunia, Kansela wa Ujermani  ameelezea  juu ya mshikamano wa Kimataifa katika nchi za Afrika na hasa zaidi zenye kipeo cha matatizo ambapo sehemu kubwa ya wahamiaji wanaokuja Ulaya. Amesema Afrika inaonekana kuwa ndiyo mpaka wa Ulaya kuanza na  kanda za Sahel. Hivyo amesema  mshikamano lazima ufanyike ili kuwezesha ujenzi wa jamii ya watu wa Afrika waweze kupata ajira na maendeleo. Ameongeza; ni lazima kupanua uwezekano ili waondokane na umaskini na kubaguliwa sehemu kubwa ya watu. Katika kuelekeza zaidi ametaja mfano wa mpango wa ambao umeanzishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, wa kuorodhesha watu katika takwimu ya Afrika uitwao “BRAVO”, hasa zaidi katika nchi ya Burkina Faso maahali ambapo wametoka watu wengi zaidi ya milioni tatu na nusu, wengi wao  wakiwa  ni watoto. Aidha Kansela Merkel amealikwa kuudhuria mkutano wa maombi  kwa ajili ya amani mwaka huu utakao fanyika katika mji wa Münster e Osnabrück Ujermani kuanzia tarehe  10 hadi  12 Septemba 2017.

Kwa njia hiyo mazungumzo yamegusa pia juu mada ya mazungumzo ya kidini : kwa upande wa Merkel amesema ,Waislam kutoka Afrika , pamoja na Makanisa ya kihistoria kama vile , wakatoliki na waluteri wanapaswa kufanya kazi pamoja kwa malengo ya kuchangia ujenzi wa jamii ya raia na kusaidia maridhiano katika dini ambazo mara nyingi wanakabiliwa na vurugugu na machafuko. Ametoa wito wa kupambana na kila aina yoyote ya itikadi kali ya dhidi ya  baadhi ya makundi ya kiislam, pamoja na aina nyingine za kikristo zinazo endelea kuzuka barani Afrika wakati  hazina mwelekeo mzuri wa kujenga amani ya mwanadamu bali kuleta mafarakano na uchochezi. Kazi ya amani na mazungumzo, imeshapata ardhi ya rutuba na ushirikiano kati ya serikali ya Ujermani na Jumuiya ya mtakatifu Egidio lakini inahitaji kuimarishwa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.