2017-04-25 15:46:00

25 Aprili ni Siku ya Malaria Duniani: Afrika inaongoza kwa vifo!


Licha ya baadhi ya ishara muhimu katika kuenea kwa maambukizi  haya makubwa na hatari , ambaye Siku ya Kimataifa ni sherehe tarehe 25 Aprili, Ripoti ya Mwaka ya Malaria iliyotolewa na shirika la Afya duniania  WHO, Desemba mwaka jana inaonesha kushuka kwa maambukizi mapya: ambapo kesi za maambukizi ya  milioni 212 mwaka 2015 na vifo 429,000 duniani kote. Pungufu hiyo ya mambukizi mapya kutoka mwaka 2010 hadi 2015 ilikuwa maambukizi asilimia 21% na idadi ya vifo kupungua kwa asilimia 29%.Haya ni  matokeo  kuthibitisha jinsi gani misaada ya kifedha kutoka baadhi ya mataifa na taasisi ni umuhimu na madhubuti sana ili kuwezesha kutekelezwaji wa  WHO.  Kwa bahati mbaya mwaka 2013-2015 wamegundua kushuka kwa matumizi ya mikakati hii (matumizi ya vyandarua vilivyotiwa dawa, njia ya utambuzi wa haraka na matibabu ya kuzuia mimba na kwa watoto chini ya miaka mitano) hasa katika baadhi ya nchi kwa uwepo wa  vitendo vya ghasia za kivita. Ni mapambano ya nyuzi 360 na kufundisha mengi sana kuokana na uchumi amani na kupambana na magonjwa.

Ni lazima kusisitiza katika kuongeza  utekelezaji wa sheria na kuzuia mikakati iliyopitishwa kufikia  hivi sasa, katika kueneza mbinu katika  nchi maskini zaidi na kupanua maslahi, ufuatiliaji na uwezo uchunguzi katika nchi ambazo hazina hatari hasa katika kuendelea kusafisha maji yanayotokea katika maeneo yenye uwezekani wa kiawango cha juu cha uenezaji.Ni hatua muhimu katika mwelekeo huu ulio tolewa hivi karibuni kwa mika 10 baada ya kutangazwa .Hatua na mwongozo wa kufuata katika kuondoa malaria wakionesha zana moja na mikakati  ya kufikia malengo. Iwapo malekezo yaliyopitishwa yatafuatwa, inakadiriwa kupunguza visa vya malaria kufikia mwaka 2020.Afrika ni bara linazidi kuongoza katika maambukizi ya malaria kwa asilimia 90% na kesi asilimia 92 za vifo. Sehemu kubwa ya watu wa Afrika wanaendelea kuteseka , kwa vifo vya watoto wadogo, ulemavu  kwa sababu ya kueneza zaidi magonjwa haya katika nchi za kimaskini. Wanao athirika zaidi ni wanawake wajawazito na watoto ,ambao hawawezi kupata huduma  za kinga au kuzuia malaria.Katika kuhamasisha janga hili taarifa pia zimeosha  kuwa kwa mwaka 2016 maambukizi ya watu  ni milioni 212 na kasi za vifo vya  watu 429,000 duniani. 

Dak. Gaiampiero Pellizzer  kutoka katika shirika la CUAM , madaktari wasio kuwa na mipaka kwa upande wa Afrika amesema , watoto ndiyo wanaathirika sana kwasababu hawajakomaa kinga zao kimwili. Kwa njia hiyo ni, mbili ya tatu ya vifo  kutokana na Malaria vinawatazama watoto wa miaka chini ya mitano.Mwaka 2015 watoto 303,000 wamekufa na malaria katika maeneo ya Afrika chini ya jangwa la Sahara; pamoja na  matokeo mazuri ambayo yamepatikana tangu mwaka 2010. Madaktari wasiyo na mipaka wanaofanya kazi Afrika wako mstari wa mbele katika kusaidia kutibu na kutoa kinga za wagonjwa walio ambukizwa na malaria.

Ikumbukwe kwamba ;Shirika la Cuam Madaktari wasio kuwa na mipaka lilianzishwa mwaka 1950.Ni Shirika lisilo la kiserikali la kwanza katika Sekta ya Afya kutambuliwa nchini Italia. Ni shirika kubwa la italia kushiriki kwa ajili ya kukuza na kulinda afya za watu wa Afrika. Shirika hili ni mungano ya madaktari na wauguzi pamoja na wasaidizi wengine wanaojitolea kuwasaidia wagonjwa katika maeneo yasiyo na huduma za kiafya hasa katika nchi zenye vita za wenyewe kwa wenyewe au maafa asilia.Ni shirika ambalo limekuwa na mipango kwa muda mrefu kwa lengo la maendeleo, hata katika hali ya dharura, ili kuhakikisha huduma bora inapatikana kwa wote.Kwa miaka ya 65, madaktari  165 wametumwa kwenda kutoa huduma zao katika hospitali, 221 ni majengo ya hosptali wanazotoa huduma, nchi 41 wantenda huduma yao, na mipango mikubwa ya utekelezaji 165. 

Leo Madaktari na Afrika Cuamm wanashrikia katika nchi saba za Afrika chini ya jangwa la Sahara ikiwa ni  (Angola, Ethiopia, Msumbiji, Sierra Leone, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda) na waendeshaji 827 ambao  (213 kutoka Ulaya  na Waafrika 614),Miradi  72 ya ushirikiano msingi na mamia  ya miradi midogo  midogo ya kusaidia hospitali 14 za wilaya 35(ikiwa ni vituo vya afya ya umma, wajawazito na huduma ya watoto, mapambano dhidi ya ukimwi, kifua kikuu, malaria na mafunzo), shule 3 za uuguzi na vyuo vikuu viwili (nchini Ethiopia na Msumbiji).  Kila mwaka takriban madaktari na wauuguzi 3,000 hujihusisha katika miradi mbalimbali kwenye nchi 70 na wengi wao hujitolea wakati wa likizo bila malipo yoyote. Kuna waajiriwa takriban 1,000. Makisio ya mwaka hufikia jumla la dola za Marekani milioni 400 na asilimia 80 zachangiwa kwa njia ya zawadi za watu wa binafsi. Inayobaki ni pesa za serikali mbalimbali au shirika za kimataifa kama UM au Umoja wa Ulaya.

Na Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.