2017-04-24 13:29:00

Hakuna nguvu yoyote ya binadamu yaweza kuzuia kurudi kwake Bwana!


Jumamosi 22 Aprili 2017 wakati Kanisa Katoliki linajiandaa kuadhimisha Jumapili ya kwanza baada ya Pasaka ambayo ni sikukuu ya Huruma ya Mungu, Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa kwa Makanisa ya Mshariki, ameadhimisha misa Takatifu kwa ajili ya Sikukuu ya Maria Mwombezi Katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Campano nchini Italia.Katika mahubiri yake Kardinali Sandri amesema liturujia ya Kanisa katika siku nane , imeadhimisha Pasaka ya Yesu,ambayo ni fumbo la ufufuko na siku nane ni kama siku moja. Na ndiyo katika mwanga wa masifu ya jioni, Aleluiya inaunganisha sikukuu ya Jumuiya yote ya Mtakatifu Yohane Campano kumsifu Maria Mtakatifu anaye heshimiwa katika Kanisa hilo. Akigusia juu ya Sanamu ya Bikira Maria inayo heshimiwa katika kanisa, kardinali amesema, Sanamu ya Maria ni sawa na maneno ya Injili yalivyosema kwamba, Yesu alikwenda katika nyumba ya mitume siku hiyo ya Pasaka akakaa kati yao wakati Tomasi hakuwepo; Na siku ya nane aliingia ndani ya nyumba milango ikiwa imefungwa akaketi kati ya mitume hao pamoja na Tomasi ambaye hakuwa anaamini ufufko wake.

Maneno hayo pia yanafanana na mwinjili Yohane mwanzo “Neno lilifanyika mwili, akakaa kwetu”, baadaye akaendelea kusema, “alikuja kati ya watu wake lakini wao hawakumpokea”…..Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili alitaka kumfikia binadamu ambaye amepotea , ni yeye wa kwanza kupiha hatua mbele kwa aliji ya kutafuta aliye potea ili kumkomboa. Na katika  barua ya kwanza ya Mtakatitu huyo anasema kuwa , “siyo sisi tulio tangulia kumpenda , bali ni yeye alitupenda akiwa wa kwanza na kumtuma mwanae”. Fumbo la Pasaka linadhibitisha kuwa Yesu hakujificha, alikwenda Yerusalem, akajiachia  akamatwe  ili yatimizwe yale yaliyo kuwa yametabiriwa na maandiko matakatifu . Yeye alikuwa mwanakondoo asiye kuwa na madoa, mnyenyekevu altareni na katika msalaba, Yeye mwenyewe alijikabidhi kwa Baba yake  na akawasamehe wadhambi na kadhalika baadaye akawapa roho yake. Kardinali Sandri amesema, Kaburi lilochimbwa katika mwamba na kifo havikuweza kumwifadhi , kwani  yeye sasa ni mzima , msulibiwa amefufuka, kama anavyo watokea mitume kuminambili ,akajionesha kwa Tomasi asiye amini. Kwa njia hiyo ndipo tunatambua kwamba hakuna hata mmoja  ataweza kuzuia kurudi kwake Bwana, hakuna nguvu yoyote ya binadamu  na wala nguvu kutoka kuzimu inayoweza kuzuia msulibiwa,ni Kristo ameshinda dhambi, mauti na shetani.

Kardinali Sandri amesema katika injili hiyo ni kumwona Yesu anakuja kati ya mitume wake kuanzia sura ya mama yake  Maria, kwa njia hiyo tutafakari jisni gani Mama Maria amekuwa wa kwanza kumpokea Kristo  na pia ni mama wa kwanza wa waamini wote. Bikira Maria wa Nazareth ndiyo wa kwanza kuchomwa mkuki kama alivyotabiri Simoni. Hiyo i kwasababu akiwa na wawake wengine na mtume mpendwa wa Yesu walikuwa pamoja chini ya msalaba, wakitazama mateso ya Yesu siku ya Ijumaa kuu. Mama Maria anatambua namna ya kuteseka lakini pia alisikia sauti ya maneno ya Yesu akisema, “Baba wasamehe hawa….” Moyo wa mama Maria ulikuwa umezoea kuwa tayari, tangu wakati wa kukutana na Malaika wa Bwana huko Nazareth,tangu alipoitikiwa “tazama mimi hapa mtumishi wa Bwana , na iwe kwangu kama ulivyonena”.Yeye hakuchanganyikiwa kama mama mwenye kudai haki kwa ajili ya mtoto wake kuhukumiwa bila hatia, Yeye ni shahidi wa haki wa Yesu akiwa anakamilisha msalabani ahadi kwa ajili ya binadamu mwenye makosa.

Mama Maria alitambua thamani ya amani kati ya mbingu na binadamu ambayo Yesu mwenyewe alilipa kwa damu yake Takatifu.Hiyo ndiyo tazama mimi hapa chini ya msalaba, ni matokeo ya moyo wake kwa aliji ya utume ulio anza tangu mwanzo na ambao unaendelea hadi mwisho, yaania atakaporudi mwokozi kuhukumu dunia. Ndiyo sauti ya Yesu isemayo “ mama tazama mwanao”… na tangu wakati huo Maria akawa mama yetu.
Kardinali amemalizia akisema;tunafikiria tendo la Yesu kufanyika mwili ni tendo la  la wakati uliopita ambao hautuhusu, na kumbe ni kinyume kwasababu , kuamini Yesu maana yake ni kujitoa sisi wenyewe kwa unyenyekevu, na ujasiri kama mama Maria. Yesu aweza kuendelea kuishi  ndani mwetu na wengine kwa maana ya kujtoa mikono yake iendelee kuwabembeleza masikini, mguu yetu iendelee kutembea kukutana na ndugu kuwasaidia waliotengwa na jamii .Ni kuendelea kufanya kazi katika shamba  la Bwana katika kuwatetea wanyonge ; akili zetu zifikiria mipango kwa njia ya mwanga wa Injili na zaidi kujitoa kwa moyo wote katika kupenda na kufanya mang’amuzi kwa mijibu wa mapenzi ya Mungu. Yote hayo yawezekana kwa njia ya Roho mtakatifu, na kwa njia hiyo sisi ni vyombo vya Mungu kwasababu Yesu anaendelea kujitoa mwenyewe katika ulimwengu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.