2017-04-22 13:36:00

Sikukuu ya Vesakh 2017: Kristo na Budha walikuwa wajenzi wa amani!


Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini wameandika ujumbe kwa ajili ya tukio la Sikukuu ya Vesakh kwa waamini wa dini ya Budha. Ni maadhimisho yafanyikayo kila mwaka mwezi wa Tano, ambapo siku hiyo inakumbusha natukio makuuu matatu ya maisha ya Gautama Budha:siku yake ya kuzaliwa, mwanga na kifo chake.Ni sikukuu inayotoa fursa ya kuwa karibu na watu wanaoteseka,ili kuwapatia faraja na furaha kwa njia ya huduma ya huruma;hivyo hata mwaka 2017,sikukuu ina malengo muhimu kwa jamii ya kuunda umoja wa kupinga vurugu na kutokutumia nguvu, kwa ajili ya kudumisha amani.

Ujumbe ulio tiwa saini na Rais wa Baraza la Kipapa kwa Majadiliano ya Kidini Kardinali  Jean-Louis Tauran unasema,mwaka huu ni kutaka kutafakari kwa pamoja juu ya haja ya  haraka ya kuhamasisha utamaduni wa amani na siyo wa kutumia nguvu. Dini ndiyo iko  katika ukurasa wa kwanza  duniani, japokuwa  wakati mwingine inakwenda kinyume. Hiyo ni kwasababu wakati waamini wengine wanajikita kuhamasisha amani, wengine ndiyo wanatafuta fursa za kutumia dini kwa manufaa yao binafsi ya kufanya vitendo vya vurugu na chuki. Tunaona matendo ya kujitoa kwa moyo ili waathirika wengi watokane na vurugu na kupona na kuridhiana,lakini pia bado kuna jitihada mbalimbali za kuzuia matendo hayo kutoka kwa wengine.
Umoja wa mshikamano wa dini kidunia unafanya kila njia lakini bado kuna sera za kisiasa kutumia dini, kuna utambuzi juu ya umaskini magonjwa ya mlipuko , njaa katika ulimwengu , na pia kuongezeka janga la utengezaji wa silaha. Hali hizi zinahitaji juhudi za pamoja kupinga kwa nguvu juu ya matumizi ya silaha na nguvu za aina yoyote.

Yesu Kristo na Budha walihamasisha hali ya kutotumia nguvu, walikuwa wajenzi wa amani. Kama anavyo andika Baba Mtakatifu Francisko kwamba, hata Yesu aliishi katika kipindi cha kutumia nguvu. Lakini Yeye alifundisha kwamba uwanja wa kweli wa mapambano ya kukabiliana na nguvu na amani ni katika moyo wa kibinadamu.Ni kwa njia ya Injili ya Mtakatifu Marko  isemayo:” maana kutoka ndani moyo wa mtu,hutoka mawazo mabaya (Mk 7,21). Katika  ujumbe wa Siku ya Amani Duniani mwaka 2017,wenye kaulimbiu “Kutotumia nguvu: mtindo wa siasa ya amani”. Baba Mtakatifu Francisko kwenye ujumbe huo amebainisha kuwa; hata Yesu mwenyewe alionesha njia ya kutotumia nguvu.Kwa maana hiyo ili leo hii kuwa mitume wa kweli maana yake ni kukubali wito huo wa kutotumia nguvu.Mwanzilishi wa dhehebu Budha alitangaza ujumbe wa kutotumia nguvu na pia  amani akiwatia moyo wote ili wawashinde wenye kuwa na chuki.Wema uweze kushinda ubaya kwa njia ya fumbo la ukarimu na tabia za uongo zishindwa  kwa njia ya ukweli. Yeye alifundisha kuwa ushindi wa adui uleta urafiki;na wale wanao shindwa ubaki na uchungu;lakini wanao shinda uishi kwa amani. Kwa njia hiyo Kardinali Tauran amesema ni jambo jema kutafuta njia hizo kwa pamoja ili kila mmoja aweza kushinda mara nyingi vita lakini  vita bora zaidi ni vile vya mtu kujishinda mwenyewe.

Halikadhalika, amebainsha kwamba, pamoja na mafundisho haya matukufu, jamii nyingi zinakabiliwa na athari za majeruhi ya zamani na sasa ambazo zimetokana na vurugu na migogoro. Jambo hili ni pamoja na unyanyasaji wa majumbani,  kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kisaikolojia, na unyanyasaji dhidi ya mazingira ambayo ni nyumba yetu ya pamoja. Ni huzuni kuona unyanyaaji unazaa matatizo mengine ya kijamii na hivyo uchaguzi wa kutokutumia nguvu uwe ndiyo njia ya maisha zaidi ni haja kubwa na haraka katika kuwajibikaji ngazi zote za kitaifa na kimataifa.(Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko 15 Desemba 2016).

Pamoja na kutambua njia pekee ya umoja wa dini zetu mbili,tuendelee kubaki na juhudi na tukubaliane kwamba vurugu zinatokana na moyo wa binadamu na pia uovu wa mtu unasababishwa na maovu ya kimuundo. Ndiyo maana sisi tumeitwa kuwa na ubia wa pamoja kujifunza sababu za vurugu, kufundisha wafuasi wetu wanaohusika jinsi gani ya kupambana na maovu katika mioyo yao. Kujikomboa madhara kwa upande wetu na hata kwa waathirika wote na wahusika wa ghasia; kutengeneza upya mioyo na akili za watu wote, hasa watoto kwa upendo, kuishi kwa amani na watu wote na mazingira.  Kufundisha kwamba hakuna amani bila haki, hakuna haki ya kweli bila msamaha; kukaribisha kila mtu kwa kushirikiana katika kuzuia migogoro katika kuijenga upya jamii iliyogawanyika.

Aidha kuhamasisha vyombo vya habari katika kuzuia na kupambana na hotuba zinazochochea chuki, na taarifa za upendeleo au kuchukiza; kuhimiza mageuzi ya elimu na kuzuia kuvuruga katika tafsiri potofu ya historia, maandiko ya kihistoria pia katika Maandiko matakatifu ; na mwisho  kuomba kwa ajili ya amani duniani ili kupata njia ya kusitisha vurugu.

Sr Amgela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.