2017-04-15 15:51:00

Ujumbe wa Pasaka 2017 kutoka Nchi Takatifu: Tuwe viumbe wapya tena!


Tunahitaji bado kuwa viumbe wapya katika mji huu ambao kila kitu utafikiri ni kujirudia kwa upya , hali ya hofu na kogopana , kutokuwa na matumaini ya zawadi . Pia hali ya kutokuwa wazi kwa kutafuta nafasi toauti kama kimbilio, linalozuia kupokea changamoto ya matumaini, urafiki ambao ndiyo ungeweza kuwa suluhisho la matatizo yetu.Ni maneno ya Askofu Mkuu PierBatista Pizzaballa, Msimamizi wa kitume katika Maeneo Matakatifu  aliyosema katika ujumbe wake kwa Padre Francesco Patton Msimamizi wa Kanisa Kuu la Yerusalem wakati wa kupeana matashi mema ya Heri ya Pasaka katika nyumba ya Kipatriaki kwenye maeneo matakatifu Yerusalem.

Katika kupeana heri na  matashi Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume katika Maendeo Matakatifu amesisitiza juu ya mahitaji ya kuwa viumbe mpya, wenye uwezo wa kupokea mambo mapya.Na ili kufanya  hivyo ni lazima pia kujua jinsi ya kufa na kujitoa maisha katika kubadili ubinadamu wa kizamani ndani mwetu. Lakini amesema kuwa anatambua jinsi ilivyo kazi ngumu hiyo zaidi, inakulazimu kuacha kutafuta zile njia ndogo gogo za usalama , au kuacha kutafuta kidogo au kikubwa ikiwa na  maana ya kutafuta umiliki kama vile wa  mali na madaraka.Askofu ameongeza kuwa ni kweli kwamba kuna ugumu wa kuondokana navyo; na kwa njia hiyo,bado tunayo kazi ya kufanya ; na ndiyo matashi mema ninayo watakia.

Ameongeza kusema hiyo ni kwa ajili ya maisha ya imani yetu na hata kwa ajili ya utu wetu,na huduma ambayo sisi wote tunahitaji na tunatkiwa kufanya.Tunapaswa kuwa na ujasiri wa kujisalimisha maisha yetu kwa Kristo, na kuruhusu nguvu ya upendo wake itukumbatie. Aidha Padre Pattoni katika hotuba yake , amesema kuwa  karibu naye  kwa ushirikiano na sala kwa ajili ya utume katika maeneo Matakatifu Yerusalem ,pia amesema kamwe tusisahau mateso mengi ya watu wetu kwasababu ya mwanga wa Pasaka bado unatoa sauti ya mwisho.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.