2017-04-11 15:44:00

Umoja wa nchi za Ulaya kusaidia nchi ya Libya katika Afya na Elimu!


Umoja wa nchi za Ulaya wataongeza msaada kwa ajili ya nchi ya Libia katika sekta ya Afya na elimu.Haya ni maneno yaliyo semwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ndani ya nchi  za kiarabu ulio fanyika nchini Libia, na mkutano huo walishiriki wawakilishi wa masuala ya elimu kutoka katika Umoja wa nchi za Ulaya hivi karibuni mjini Tunisi.Halikadhalika taarifa zinasema, Umoja wa nchi za Ulaya mwezi ujao watafungua mpango wa Zahanati katika miji wa Tripoli , Bengazi, Zliten na Gharan.Hii ni sehemu mojawapo ya mpango mkubwa inaotazamiwa kuwekeza karibia milioni 10 za dola za kimerekani. Vituo vya afya vinategemewa kujengwa wodi ya wanawake wajawazito, ya watoto wanye ulemavu wa akili,wa  magonjwa yasiyo ya kuambukiza na maabara ya kupima damu.

Hayo yamesema na  mwakilishi wa Umoja wa nchi za Ulaya kwa ya nchi ya Libia , Bettina Muscheidt. Milioni 6 dola ya kimarekani , zitaweza kuzindua miradi kwa upya na kusimamia huduma ya afya iliyokuwa imesitishwa tangu mwaka 2014 kutokana na mapambano dhidi ya makundi mbalimbali ya wanangambo yanayokabiliana na nchi hiyo. Kwa upande wa elimu, Umoja wa nchi za Ulaya watazingatia hasa kwa kipindi cha kwanza juu ya ukarabati wa baadhi ya maeneo .Kwa namna ya pekee wanategemea kuanza na ukarabati wa Chuo Kikuu cha Sirte na Bengasi. Katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani ya nchi za Urabni huko Libia ulio kuwa unaongozwa a mada kuhusu mafunzo  wakiwepo pia wawakilishi na wataalamu wa elimu wa Umoja wa nchi za Ulaya,wamekubaliana kukamilisha mpango huo katika mwezi wa Ramadhan.

Pamoja na hayo lakini hali bado ya nchi inakabiliwa na channgamoto kubwa ya watu wanao endelea kukimbia na kukabiliana na safari ya hatari, kwamfano rtaarifa zinasema hivi karibuni kumetokea mapambano kati ya dolia wa fukweni na waalifu wanao tumia mitumbwi kuafirisha watu kwenda Ulaya. Katika mapambano hayo, walifu 4 wamekufa na mmoja kupotea majini wakiwa wamepakia watu wengi katika mtumbwi wakielekea Ulaya.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.