2017-04-10 16:50:00

Tarehe 12 Aprili 2017 Siku ya Maombi kwa ajili ya nchi ya Siria!


Caritas nchini  italiana kwa ushirikiano na  Pax Christ wametoa wito wa kufanya siku ya kufunga kwa maombi  kwa ajili ya nchi ya Siria. Siku hiyo ya kufunga kwa maombi  itafanyika tarehe 12 Aprili 2017, tutakuwa tunaanza mkesha wa Siku tatu Kuu kabla ya pasaka. Ni siku ambayo isisahulike ya kushiriki mateso ya  Kristo katika mwanga wa matumaini ya Pasaka.

Taarifa kutoka ofisi ya Caritas ya italia na Pax Christ wanakumbusha kwa namna ya pekee maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ibada ya misa ya tarehe 13 Septemba 2014 akisema, hata leo waathirika ni wengi. Je hiyo inawezekanaje?. Inawezekana  kwasababu matokeo mengi yaliyoko nyuma yetu tusiko kuona ndipo kuna mafao ya wengine wenye mipango yao ya kisiasa , kwa kupenda mali, fedha na madaraka na pia kuna viwanda vya silaha vinavyo onekana kuwa muhumu kwao.Ni jambo linalozidi  kutishia kwani hao wana andaa machafuko maana wanaotengeneza silaha wamekwisha andika katika mioyo yao kwamba hao wanatuhusu nini?Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana siku ya Jumapili ya Matawi tarehe 9 Aprili 2017 kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro amerudia kusema maneno hayo na wito juu ya tukio la mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea  nchi ya Sweden na Misiri. Amemwomba Mwenyezi Mungu ili aweze kuongoa nyoyo za watu wanaojenga hofu na utamaduni wa kifo pamoja na wale wote wanaotengeneza na kufanya biashara ya silaha duniani.

Taarifa pia Caritas ya Italia zimekumbusha juu ya tukio la siku za hivi karibuni huko Idlib nchini Siria, ambap watu wengi wamajeruhiawa na wengine kufariki wakwemo watoto wengi katika shambulio linaloshukiwa kuwa la kemikali. Katika vita ukweli ndiyo kwanza unathirika na hivyo  Caritas ya Italia na Pax Christ wanasisitiza na kuomba kwa sauti moja ili vyombo vinavyo husika watafute namna ya kusitisha vita hivi, ili kuweza kuzuia kile kinacho weza kuitwa vita ya tatu ya dunia. Ni mwaliko kwa wote kushiriki katika maombi kwa ajili ya waathirika wote duniani na pia kuwaombea wenye kusababisha vita hivyo, vikiwemo zilaha za aina zote na hata nyuklia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.