2017-04-09 12:25:00

Tunahitaji vijana wanao kimbia kwa haraka mfano wa Mama Maria


Jumamosi Jioni tarehe 8 April 2017 Baba Mtakatifu aliungana na vijana wa Jimbo kuu la Roma walio unganika na  vijana kutoka Pande zote za Dunia  kwenye Mkutano wa Kimataifa kwa maandalizi ya Siku ya Vijana Panama ijayo kufanya mkesha wa Maombi kabla ya Jumapili ya Matawi.Wakati wamahubiri yake ameanza  kuwashuru uwepo wao , ikiwani mwanzo wa safari ya kuelekea Sinodi ya Vijana yenye kuwa na kauli mbiu Vijana imani na utambuzi wa miito, kwa maana nyingine yeye amependelea kusema kwa kirahisi kwamba ni Sinodi ya vijana , kwani inaeleweka vema, pia  sehemu pili ikiwa ni safari kuelekea Panama,amemgeukia Askofu Mkuu wa Panama na kumsalimia.

Tumesikiliza Injili, tumesali, na kuimba: tumepeleka maua kwa Mama Maria, na pia kuchukua msalaba ambao unatoka Cracovia, maana , Jumapili ya matawi utakabidhiwa  vijana wa Panama. Kutoka Cracovia kwenda Panama kati ya Sinodi. Ni sinodi ambayo hakuna kijana yoyote anayebaguliwa , na hata kujisikia mpweke .Sinodi siyo kwa ajili ya wakatoliki, au vyama vya vijana katoliki , hapana . Sinodi ni kwa ajili ya wote, kwani vijana wako mstari wa mbele.Hata vijana wasio pendelea dini ,walio kwenda mbali na Kanisa , na hata wale wanao jisikia kutomkujua Mungu kabisa , kwasababu Sinodi hiyo ni kwa ajili ya vijana , na wote tunataka kuwasikiliza . Kila kijana ana jambo la kueleza kwa wengine, kuwaeleza watu wazima, mapadre, watawa, maaskofu hata papa; wote tuna mahitaji ya kusikiliza Vijana , Baba Mtakatifu amesisititiza.

Katika kukumbuka Msalaba , Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha maneno aliyo waeleza huko Cracovia katika Siku ya Vijana Duniani 2016  , kwamba siyo jambo jema  kumuona kijana anakwenda pensheni akiwa na miaka 20i,  ni mbaya kumuona kijana anaishi au kukaa katika sofa bila kujibidisha . Siyo kweli kijana kwenda pensheni, wala  kukaa katika sofa. Ni kijana anayepaswa kuwa katika mwendo , ni kijana anaye paswa kuwa barabarani, kuendelea  mbele akiwa na wengine, kwa kutazama maisha endelevu.Injili ya Mtakatifu Luka (Lc 1,39-45) wakati Maria alipokea zawadi ya wito mkubwa wa kubeba  zawadi ya Mungu kwa ajili yetu, na wakati huo akapokea habari kuwa binamu yakeni  mzee anamsubiri mtoto , alikuwa anahitaji msaada ,Maria aliondoka kwa haraka.Kwa haraka ina maana ya dunia ya leo inahitaji vijana waende kwa haraka , wasichoke  kwenda haraka, vijana wanao jisikia  wito wa kutoa maisha katika utume. Baba amesema hayo kwa  hayo kwa kutoa mfano wa Mtawa Maria Lisa aliye toa ushuhuda ya kwamba ni kijana katika safari.

Katika ushuhuda wake  ameeleza juu ya uzoefu wake, huo ni uzoefu  wa safari. Tuna haja ya vijana katika safari. Dunia inaweza kubadilika iwapo tuna vijana katika safari. Japokuwa kuna changamoto ya kipeo cha ukosefu wa ajira unao wakumba vijana  wa leo, na kwa bahati mbaya wanabaguliwa : hawana kazi,hawana mfano wa kufuata , kwasababu hawana  elimu wanakosa kushirikishwa. Vijana wengi wana lazimika kukimbia na kuhamia nchi nyingine .Baba Mtakatifu amesema hiyo ni ngumu kutaja  lakini ki ukweli  vijana wamekuwa bidhaa ya kubaguliwa! Anaendelea ;Kwa njia hiyo sisi hatuwezi kuacha namna hii , tunalazimika kufanya Sinodi, kwa ajili ya kusema sisi tuko hapa na tunakwenda Panama kusema sisi vijana tuko njiani na hatutaki kuwa bidhaa za kubaguliwa maana  tunayo thamani ya kutoa.

Aidha amesema kwamba amefikiria wakati Kijana Pompey  anatoa ushuhuda wake ,na kusema yeye ameathirika mara mbili kama bidhaa ya kubaguliwa akiwa na miaka 8 na sasa ana miaka 18, lakini ameweza kufanikiwa. Amekuwa na uwezo wa kuamka .Ameongeza kuseam ,tukitazama upeo wa maisha daima yanatushanganza   kama alivyo toa ushuhuda sisita Maria Lisa, na pia Pompey.Wote tuko njiani kuekea Sinodi na Panama. Katika safari kuna hatari zake , lakini kama Kijana hajiweki katika hatari amezeeka , na hivyo tunapaswa kujihatarisha.Sista Maria Lisa amesema mara baada ya Kipaimara alikwenda mbali na Kanisa, Babab Mtakatifu Francisko ametoa mfano kuhusiana na hilo kwamba, mnatambua nchini Itala Sakramenti ya Kipaimara wamezeoa kuitaja kama Sakramenti ya ”kwaheri ya kuonana” , kwasababu wengi mara baada ya kupata kipaimara hawarudi tena Kanisani.

Ni kwasababu gani hiyo?, kwasababu vijan wengi hawajuhi nini cha kufanya , lakini Maria Lisa alisimama na kutafakari japokuwa alikuwa katika mwendo… Mara nyingi katika safari ya giza nene  na unakosa mwanga , mawazo , au unayo mawazo lakini hutambui lolote, na mwisho wake yeye aliweza kufanikiwa. Nyinyi vijana mnapaswa kujiweka hatari ya maisha , kwasababu leo hii mnapaswa kuandaa maisha ya baadaye kwa maana maisha endelevu yako mikononi mwenu !Ndani ya Sinodi inataka wakuwasiliza vijana, wanafikira nini,wanasikia nini, wanataka nini , wanakosoa nini , je ni kitu gani wanajutia. Yote hayo Kanisa linahitaji kujirudi upya na ni msimu mpya wa vijana. 

Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko anawaalika katika safari hii kuelekea Sinodi na Panama ili ifanyike kwa furaha  , kwa kufanya hivyo na matarajio bila kuwa na hofu, bila aibu na kwa ujasiri.Inahitaji ujasiri na kujaribu kuchukua yale mazuri katika mambo madogo madogo kama Pompey alivyosema kwamba ni “kuyachulia hayo mambo madogo na mazuri ya kila siku na kushukuru kwa jinsi ulivyo , kwa maana mimi ndivyo nilivyo.” Ameongeza Baba Mtakatifu, mara nyingi tunapoteza muda kujiuliza mimi ni nani, ukifanya hivyo itakuwa ni kwa maisha yako yote, jambo la kujiuliza Baba Mtakatifu anashauri kwamba Mimi nipo kwa ajili ya nani. Kama vile alivyo jalivyojiuliza mama yetu Maria, wakati huo ilikuwa ni kwa ajili ya binamu yake na alikwenda. Hivyo ni kusema kwamba tunapaswa kujiuliza nipo kwa ajili gani na siyo mimi ni nani maana hiyo inakuja baadaye, tunapasawa kufanya kazi ya kufikiria katika lugha tatu ya akili, moyo na mikonoili kupata kuweza kwenda mabele daima.

Jambo nyingine Baba Mtakatifu amesema , Sinodi siyo ukumbi wa mazungumzo na Siku ya vijana haitakuwa ukumbi wa mazungumzo , au ukumbi wa sanaa za michezo, jambo zuri,na baadaye kwaheri ya kuonana, Siku ya vijana inahiji matendo halisi, Maisha yanatualikwa kufanya matendo ya dhati, katika  utamaduni ulio mdhaifu, inahitajika matendo ya halisi,uhalisia wa wito wenu, amesisitiza Baba Mtaktifu Francisko. Mwishoni amewapa kazi ya kufanya akisema kwamba Kanisa linawaomba  wafanya utume, utume huo  ni kuongea na wazee ,kufanya mazungumzo na wazee kati ya vijana .Nabii Yoeli (3,2) amesama juu ya unabii , kwamba ”wazee watakuwa na ndoto, na vijana watatoa unabii” , kwa maana watachukua kazi ya kinabii kwenda mbele ni unabii wa mambo halisi. Hiyo ndiyo kazi ninayo wapatia ninyi kufanya kwa jina la Kanisa kwenda kuzungumza na wazee . Lazima kuongea nao, kuwauliza mambo.Fanyeni kwamba ndoto zao mnazichukia kwenda mbele ili mpate kutoa unabii katika safari yenu na kutenda mambo halisi ya kinabii.Hudi ndiyo  utume wenu wa leo ambao Kanisa linawaomba kufanya. Sijui  kama mimi nitakuwepo, lakini kwa hakika Papa atakuwepo Panama na atawauliza maswali hayo kama mmepata kuongea na wazee.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.