2017-04-09 15:47:00

8 Aprili ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Waromania!


Baada ya salama zake Karidinali Turkson na pia kupata fursa ya kuchangia kazi ya Kanisa na Baraza lake la Huduma ya maendeleo ya binadamu kamili kwa kuwatazama hata watu  wa Romania,kwa uwepo hata wa Mwakilishi wa Kipapa katika Nchi ya Hungry Balozi  Eduard  Habsburg-Lothringen.
 Amewashukuru kufanya Mkutano huo wakati ulikuwa ni mkesha wa Siku ya Kimataifa ya utambuzi waromania, ili serikali ya  Hungary iliyopewa majukumu ya kushikiria Unyekiti wa Umoja wa Nchi za Ulaya kutoa mchango  wake kwa ajili ya kuwashirikisha kijamii watu hawa. Kardinali Turkson amesema kushirikisha kijamii, na huduma ya kichungaji kwa Waromania ni masuala mawili muhimu yanayo ungana pamoja , kutoka katika historia, pia changamoto ya Kanisa , kijamii na hata ya Jumuiya hawa Waromania.

Kabila hili pamoja na kuwapo kwa miaka mingi  Barani Ulaya,lakini bado ni   sehemu ndogo ya watu , ambao wanabaguliwa na kunyiwa haki msingi za binadamu. Mkataba wa Kimataifa juu ya  Haki za binadamu, zinasema ni “kuhakikisha kwamba kila binadamu kama mmoja wa jamii , anao wajibu wa kuwa na haki za kuchumi, kijamii na utamanduni ,msingi na kuheshimiwa utu wake, uhuru wa kuendelea na kukuza nafsi yake”.
Kwa bahati mbaya Kardinali Turkson amesema kuna sababu nyingi,  ambazo hawa waromania hawapati haki zao , hawapati msaada  kutoka katika vyombo vya kisheria ili kuhamasisha maendeleo katika mantiki nyingi za uwepo wao. Zaidi ya hayo wanakumba na kubaguliwa, kutengwa, kunyanyaswa kutokana na vigezo vya matukio yanayozidi kuongezeka katika jamii hadi kufikia vurugu na migogoro.

Hivyo ni namna gani ya kuwasaidia : Pamoja na hayo mateso  makali wanayokumbana nayo katika historia, bado ni watu wenye utajiri mkubwa katika maisha na tamaduni zao. Kwa njia hiyo Waromania wanapaswa kusaidiwa kuweza kuishi vyema na kushirikishwa kikamilifu katika mfungamano wa kijamii. Wasaidiwe kupata fursa za ajira na kwa upande wa Makanisa, wawahudumie kikamilifu katika maisha yao ya kiroho kwa kuwa na mikakati bora. Wapewe elimu itakayowakomboa katika umaskini na ujinga. Watendewe mema na kupewa haki zao msingi. Wakristo wawe ni mfano wa Msamaria mwema, kwa kutenda na kutekeleza yale ambayo Yesu anawatuma kufanya na kwa njia hii, kweli Wakristo watakuwa ni ndugu na jirani wa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Katika hotuba ya Baba Mtakatifu  Francisko ya tarehe 26 Oktoba 2016 alisistiza juu ya kuwa na mshikamano, ushirikiano ili kuondoa tabia za ubaguzi wa rangi , na kwamba asiwepo mtu yoyote anayebaguliwa na kujisikia pweke. Aidha alitoa  wito kwa wote wanao husika ya kukuza na kuheshimu binadamu aweze kufurahia mambo msingi na hasa haki zake. Vilevile wito juu ya kuwa na mazungumzo ya kweli ambayo hujenga udugu kwa urahisi na ndiyo njia ya kuweza kutunza uzalendo, utamaduni na adhi ukiwa ndani ya nchi nyingine hasa inayojali  namna ya kushirikisha.
Kwa mtazamo wa upeo wa binadamu wa Kanisa linalopenda kujikita hasa kwa masikini Kanisa linafikiria huduma ya kichungaji katika Kabila hili bila kusita. Kanisa linamtazama kwa kila mtu kwa kujali , kukuza utamaduni wake, uzalendo , namna ya kifikiri na mavazi. Kanisa linawajibika kufanya huduma ya kichungaji , kwa mantiki ya kiroho, kisakaramenti, liturujia ya maisha, hata kwa upande wa Jamii na matendo ya huruma, aidha kutetea haki za binadamu , na hasa kwa upand wa elimu na mafunzo na ajira. Kawa namna hiyo linajikita katika kutoa huduma ya watu hawa kwa njia ya mapadre wengi , watawa na walei wa kujitolea.

Aidha Kardinali amemtaja Mwenye heri mpya  mwenye asili ya kabila hili Emilia Fernández Rodriguez aliyetangazwa tarehe 25 Machi 2017 huko Armenia Huispania. Siku ya Kimataifa ya Waromania, inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 8 Aprili kwa kutambua kwamba, uwepo wao ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wanapaswa kulindwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa na kamwe wasibezwe wala kuteswa kama inavyojionesha sehemu mbali mbali za Ulaya. Hii ni siku inayo andaliwa na shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya CCEE kwa kushirikiana na Shirikisho la Makanisa ya Kiangalikani Barani Ulaya CEC.

Kardinali Turkson amemalizia kwa kukumbusha maneno ya Baba Matakatifu Francisko anayesema kwamba ni roho ya hurumainayotualika kupambana kwa ajili ya utetezi wa thamani ya watu hawa waromania .Hivyo Injili ya Huruma iweze kufungua nafsi ya mioyo na mikono kwa ajili ya wahitaji zaidi walio pembezoni na kubaguliwa kwa kuanzia wale walio karibu nasi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.