2017-04-06 16:53:00

Baba Mtakatifu kufanya Maadhimisho ya Alhamisi Kuu gerezani


Tarehe 13 Aprili 2017 Baba Mtakatifu Francisko atakwenda katika nyumba ya wafungwa kwenye Wilaya ya Frosinone na Jimbo la Palestrina Italia kuadhimisha Misa ya Alhamisi Kuu, ikiwa ni pamoja na Liturujia ya kunawisha miguu ambapo ataweza kuwanawisha miguu  baadhi ya wafungwa. 
Alhamisi kuu ni sikukuu ya Ukristo inayoadhimisha  ile karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake kabla hajakamatwa na kuhani mkuu wa Israeli.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu katika kuonesha ukaribu wa wale walio nje ya ulimwengu kama wafungwa hata mwaka huu anatoa utashi huo  tunapoingia katika wiki kuu katika ufunguzi wa siku tatu kuu  kabla ya Pasaka ambapo atakwenda katika nyumba ya wafungwa Paliano na kusheherekea Karamu kuu ambayo inaambatama na tendo la kunawisha miguu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.