Asubuhi ya tarehe 5 Aprili 2017 Baba Mtakatifu Francisko kabla ya katekesi amekutana
na kuzungumza na wawakilishi wa Viongozi wa Kiislam kutoka Uingereza katika Ukumbi
mdogo wa Mwenyeheri Paulo VI mnji Vatican.
Viongozi hao wako Roma katika tukio la Mkutano kuhusu kushirikishana, elimu na kutuma
nguvu. Aliye waongoza no Askofu wa Westminster , Kardinali Vincent Nichols,ambaye
ametoa salam baada ya utangulizi wa Kardinali Jean - Louis Tauran, Rais wa Baraza
la Kipapa wa mazungumzo ya kidini.
Kardinali Nichols akiwa ameongozana na viongozi wanne kutoka Jumuiya ya Kiislam ya
Ungereza,kama wawakilishi wa matawi yao ya Sunni na Shia,Kardinali amesema wanafanya
kazi kwa pamoja kwa ajili ya amani na mazungumzo ya kidini. Aidha kardinali amesema
Papa ni mfano halisi wa kiongozi wa wote. Vilevile amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko
kwa ujumbe wake alio utoa mara baada ya shambulio la kigaidi , na kusema kwamba shambulio
hilo kwa wakati huu linawakilisha changamoto kubwa, kutokana na hilo kwao ni fursa
ya kutoa sauti ya pamoja kwa ajili ya muungano wa nchi , kwa ajili ya amani na imani
kwa Mungu.
Na baada ya hotuba ya Kardinali, Baba Mtakatifu naye ametoa hotuba fupi kuhusiana
na mkutano huo , akisema anayo furaha kwa ajili hiyo na pia mesisitiza juu ya kusikiliza
, na hasa katika mazungumzo ya kidini , jambo kubwa na muhimu ni kusikiliza. Amebainisaha
kuwa haiwezekani kufanya mazungumzo juu ya dini kama hakuna utambuzi wa imani binafsi.
Mazungmzo ya kidini yana anzia daima na imani binafsi.
Baadaye kuna changamoto za hapa na pale kwa mfano wa asiye amini ninavyo amini au
kuishi kama ninavyoishi na akaongeza hiyo siyo lazima awe adui, bali ni ndugu wa kutembea
njia nyingine na mwingine njia ya Mungu. Vile vile kuna changamoto ya ukosefu wa
ukweli.
Mazungumzo ya kidini siyo mkakati , bali ni mazeozi ya dini ya binadamu mbele ya Mungu na mbele ya wenzake katika ubinadamu kwasababu sisi sote ni mahujaji kulekea ukweli.Kwa njia hiyo Baba mtakatifu Francisko amesema kwamba anapenda kutafakari kazi muhimu inayo paswa kufanyika leo hii kati yetu binadamu na hasa kazi hiyo ni ya sikio, kwa maana ya kusikiliza bila kuwa na haraka ya kutoa jibu.Maana yake ni kupokea neno kutoka kwa ndugu kaka na dada ndipo baadaye unafikiria kutoa yako binafsi. Lakini uwezo wa kusikiliza ndiyo muhimu sana, Baba Mtakatifu ametoa mfano na kisema inapendeza kuona watu wenye uwezo wa kusikiliza wengine, wanapokuwa wanaongea, hawatoi sauti kali. Wanaongea kwa sauti ya upole…tofauti na wale wasio kuwa na uwezo huo, kwani wanaongea kwa sauti kubwa na hata kupayuka.Ka njia hiyo kati yetu ndugu tunapaswa kuongea kwa taratibu na kwa utulivu,katika kusikiliza ili kutafuta njia ya kutembea pamoja.Tunapotambua kusikiliza na kuongea tayari ndiyo njia tuliyomo.
Viongozi wa Kiislam walioshiriki mazungumzo na Baba Mtakatifu Francisko kutoka Uingereza walikuwa Rais wa Baraza la Kiislam Uingereza, Ali Raza RIZVI: Muhammad Shahid RAZA, mwenyekiti wa jukwa la waislam Uingereza ; Shaykh Ibrahim MOGRA, Msaidizi wa mwenyekiti wa Jukwaa Wakristo na waislam Uingereza; na Sayed Ali Abbas RAZAWI, Mkurugenzi Mkuu wa chama cha Scoltland cha Ahlul Bayt .
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |