2017-04-05 08:52:00

Je nina vaa msalaba nikiwa na utambuzi wake?au kama kidani?


Ukombozi unakuja kwa njia ya  Fumbo la Msalaba.Hakuna ukombozi unaotokana na fikra tu, hakuna ukombozi wa kufikiria kama vile ndiyo matashi mema,au ti katika kufanya kwa nia njema.Ukombozi ni kwa njia ya Kristo msulibiwa tu. Kama nyoka wa shaba, maana yake mwenye uwezo wa kuchukua sumu ya dhambi na kuponya.Hayo ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne 4 Aprili 2017 wakati wa mahubiri yake katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican.

Amesema ni nini maana ya Msalaba kwetu sisi,? anauliza na kujibu kwamba ni ishara ya wakristo. Lakini sisi mara nyingi tunafanya ishala ya msalaba japokuwa hatuifanyi vizuri, ni  kwasababu hatuna imani ma  msalaba huo. Na mara nyingine  watu wengi wanafanya hivyo kwasababu ni kasumba, na utawasikia wakisema, mimi ninavaa msalaba ili watu waone mimi nilivyo mkristo.Ndiyo ni jambo jema lakini isiwe kasumba bali iwe kumbukumbu kwa yule aliyejitwisha na kubeba dhambi.Mungu alimwambia Musa: atakaye tazama nyoka atapona, na Yesu akawambia maadui wake, mtakapomtundika mwana wa binadamu, ndipo mtatambua yeye ni nani. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza;asiye tazama msalaba kwa imani atakufa na dhambi zake , na hatapokea ukombozi .

Leo hii Kanisa linatualika kufanya mahojiano juu ya fumbo la msalaba, kwa njia hiyo Mungu amekuwa mdhambi kwa ajili ya dhambi zangu.Na kila mmoja anaweze kusema ni kwa ajili yangu.Ametoa baadhi ya maswali ya kujitafakari akisema tunaweza kufikiria ni kwa njia ipi ninachukua msalaba,ni kwa njia ya kukumbuka? Je ninapofanya  ishara ya msalaba,ninautambuzi wa kile ninachofanya? Nina vaa msalaba namna gani?. Kama mimi ni mmoa wa kikundi cha dini je msalaba nina ubeba namna gani ? je ninauvaa  kama vile kidani au kama vile kito cha thamani au kama mawe ya thamani na dhahabu? Nimejifunza kubeba msalaba mahali ambapo panaumiza? Kila mmoja wetu leo hii atazame msalaba,atazama Mungu ambaye amekuwa mdhambi kwa ajili yetu sisi na atakufa  kwa ajili ya dhambi zetu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.