2017-04-03 15:53:00

Sisi sote ni wadhambi,tumtazame Yesu anaye hukumu kwa huruma


Mbele ya dhambi na ufisadi , ni Yesu Peke yake mwenye kuwa na ukamilifu  wa Sheria. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake Jumatatu 3 Aprili 2017 kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican, akichambua Injili ya siku ya Mtakatifu Yohane ,baada ya kumleta mbele yake mwanamke kahaba. Na Yesu aliwajibu “asiye kuwa na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe”.Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba hata somo kutoka katika kitabu cha Nabii Danieli limeeleza  juu ya mwanamke Susana aliyekuwa amesingiziwa na wazee wawili wanasheria, hadi kumhukumu kifo. Susana alikuwa amelazimishwa achague kati ya uaminifu kwa Mungu na Sheria, ili aokoe maisha yake: Lakini yeye alikuwa mwaminifu kwa mme wake , hata kama alikuwa ni mwanamke mwenye dhambi nyingine , kwasababu wote tu wadhambi, na asiye kuwa na dhambi ni mmoja yaani Mama Maria. Anaongeza Baba Mtakatifu  Francisko akisema, katika matukio hayo mawili yanakutana na mambo haya  kutokuwa na hatia , uasherati na sheria, kwababu katika matukio hayo mawili waamuzi walikuwa na uozo.

Na hiyo ni kwa sababu daima kumekuwa na nahakimu wafisadi ,hata leo katika sehemu nyingi za dunia wapo wengi. Je ni kwanini mtu anakuwa hivyo fisadi? Ni kwasababu ya dhambi , kwa mfano mimi ni mdhamni nimeangua na siyo mwamaminifu kwa Mungu, bali ninafayatufa namana ya kujisawazisha kwa Bwana , japokuwa unatambua siyo vema.Anaongeza Baba Mtakfifu akisema usifadi ni mahali ambapo dhambi unazidi kuingia ndani ya nafsi bila kuacha nafasi hata ya hema iingie.Yote hayo uwa ni dhambi na ufisadi pia. Wafisadi wanaamini bora kutoa hukumu ndiyo jambo zuri. Hiyo ni kwa upande wa mwanamke Susana, ambaye alihukumiwa na wale wazee wenye dhambi za usharati wakitoa ushaidi wa uongo dhidi yake.

Baba Mtakatifu Francisko anasema siyo kesi ya kwanza, kwani katika Biblia tunakutana na shuhuda za uongo kama hizo. Anakumbusha, Yesu mwenyewe, alihukumiwa kwa ajili ya shuhuda za uongo . Kwa upande wa mwanamke mzinzi tunakutana na mahakimu wa namna hiyo,kwasababu ya kukuza tafsiri ngumu ya sheria . Sheria za wakati ule hazikutoa nafasi  ya Roho Mtakatifu , walikuwa mafisadi kisheria , dhidi ya neema .
Lakini kulikuwa na Yesu Mwalimu wa sheria mbele ya mahakimu wa uongo ambao walikuwa wagumu wa mioyo. Wlikuwa wakitoa hukumu zisizo za haki , na  kuwanyima watu wasio na hatia na kuwaruhusu watu wasio stahili.Yesu alisema maneno machache, kwamba asiye kuwa na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe, pia  akamwambia mwanamke kahaba kwamba haya mimi sikuhukumu, bali enda  na usitende dhambi tena. Huo ndiyo ujazo wa sheria , na wala siyo kama wa waandishi na mafarisayo ambao walikuwa ni mafisadi, walikuwa wametunga sheria nyingi, bila kuacha hata nafasi ya huruma . Yesu ni ujazo wa sheria , na Yesu anahukumu kwa huruma.

Tukiachana na  mwanamke asiyekuwa na hatia ambaye Yesu anamwita mama, Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba ni mama yake Yesu  peke yake asiyekuwa na hatia. Na kwa upande wa mahakimu wazee, Nabii anawaita kwa maneno yasiyo mazuri akisema nyinyi mlio zeeka katika uovu, inatufanya tufikirie juu ya uovu kwamba ndiyo uovu wetu tunao hukumu watu wengine.Hivyo hata sisi tunawahukumu wengine katika mioyo yetu, hata sisi ni wafisadi au hapana?. Inabidi tusimame na kutafakari . Tumtazame Yesu anaye hukumu kwa huruma akisema hata mimi sikuhukumu nenda kwa amani na usitende dhambi tena.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.