2017-04-03 16:15:00

Kumbukumbu ya Mt. Yohane Paulo II ni hai kwa waamini duniani


“Mtakatifu haraka”, ni sauti zilizo sikika kwa zaidi milioni tatu ya mahujaji walikuwapo siku ya mazishi ya Baba Mtakaifu Yohane PauloII katika viwanja vya Mtakatifu Petro . Baada ya miaka 6 akatangazwa Mwenye heri na Baba Mtakatifu Benedikto XVI ,na tarehe 27 Aprili 2014 Baba Mtakatifu Francisko akamtangaza kuwa Mtakatifu. Tangu kifo chake matamshi ya "mtakatifu haraka", imepita miaka 12 .
Ilikuwa tarehe 2 Aprili 2005 baadaya ya saa tatu na nusu za usiku Baba Mtakatifu Yohane Paulo II akaitwa na Baba Mungu,wakati anaaga dunia, tayari ulikuwa ni mkesha wa sikukuu ya Huruma ya Mungu . Tangu siku hiyo hadi mazishi yake tarhe 8 Aprili 2005 mamilioni ya mahujaji walifika kutoa salam zao za mwisho,watu hawakuchoka kusimama katika foleni hadi masaa 24 ya kuweza kuingia ndani ya Kanisa Kuu kutoa heshima zao za mwisho.Itakumbukwa pia mara yake ya mwisho kuonekana katika dirisha la Uwanja wa Mtakatifu Petro ulikuwa ni tarehe 30 Machi 2005, japokuwa hakuweza kuongea, lakini alisikika akivuta pumzi kwa nguvu na baada ya siku 3 akiwa na miaka 84 akarudi kwa Mungu Baba.

Baba Mtakatifu  Yohane Paulo II ametawala kwa  kipindi kirefu tangu mwaka 1978 hadi 2005.Kumbukumbu ya Mtakatifu Yohane Paulo II, leo hii ni hai kabisa kwa watu na pia kuwapo uwiano kati ya Papa huyo aliyesema anatoka mbali na wasasa aliyesma anatoka katika kona ya dunia.Ili kueleza  juu ya mtazamo wa watu katika uongozi na uchungaji wa  Mtakatifu Yohane Paulo II mwandishi wa habari amekutana na Askofu Vincenzo Paglia Rais wa Taasisi ya Kipapa  ya maisha na Mkuu wa Taasisi ya ndoa na familia ya Yohane Paulo wa Pili.Askofu Mkuu Paglia amesema , tuko mbele ya ushuhuda mkubwa wa kikristo unaozidi kujitambulisha kwa ngazi zote kufikia ulimwengu mzima na ambao unaonekana  katika mwanga wa utawala wa Baba Mtakatifu Francisko.

Huo pia unaweza kuelezeka vizuri kutoka katika kisima cha pamoja , kwani kuna jambo la kushangaza juu ya  Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kuwa wa  kwanza kufungua Sinodi ya kwanza ya Familia ,suala hili pia kufanyika na Baba Mtakatifu Francisko, kwa sinodi ya kwanza juu familia. Kwa njia hiyo ni vizuri kuona mambo haya muhimu mawili yanavyo ungana kwa pamoja kwa maana ya mada hiyo ni kama maendeleo na siyo mashindano bali katika ukuaji. Kwa kukuza hilo ni kuanzia na wosia wa Furaha ya upendo , ambapo kuna  mwendelezo ambao unapaswa kugunda na kuupokea kama utajiri wa nyaraka za kipapa kwa miaka ya hivi karibuni.Askofu Mkuu Paglia amesema juu ya mtazamo wa watu wa Mungu na wataalam kwa kulinganisha utawala wa Mtakatifu Yohane Paulo II na wasasa akibainisha kwamba,inapaswa kutazama uongozi wao kwa njia ya uaminifu  yaani watu wa Mungu wanavyo pokea mahusiano ya uongozi wao pamoja na utofauti wao uliopo.

Amesema hayo  akitazama mwaka mmoja baada ya wosia wake wa Furaha ya upendo.Waamini wengi wameupokea na kutafsiri kwa namna yao, kwa maana ya kuupokea kwa furaha,kama walivyokuwa wamepokea kwa furaha mafundisho juu ya familia ya Mtakatifu Yohane Paulo II na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.Lakini pia kuna kukua kwa utambuzi wa watu kwa kile wanachojua kwa mfano  ukuaji mahusiano ya kiekuemeni na mazungumzo ya kidini. Yapo mambo mengi halisi ya kutazamwa kwa umakini.Halikadhalia Askofu Muu Paglia anakumbuka zaidi mara baada ya Mtakatifu Yohane Paulo IIkufanya ziara yake nchini Brazil, kwa maneno aliyo waeleza Jumuiya ya Mtaktifu Egidio.Kwani alipata mshanagao mkubwa kuona watu wengi masikini wanaishi katika pembezono ya mji wa Braziò na hivyo anasema tukio kama hilo ndilo Mtaguso Mkuu wa Vatican II unataka kwamana Kanisa linachagua watu wote lakini zaidi ni masikini.

Aidha akitazama utume wa. Mtakatifu Yohane Paulo II juu ya shahuku ya kutembelea sehemu zilizokuwa na matatizo ya vita ghasia na vurugu, amesema kwamaba yeye mwenyewe alitaka kutembelea miji mikuu ya Zagabria, Sarajevo na Belgrado., nchi ambazo zimekuwa na matatizo makubwa ya vita hada leo. Haikuwezekana lakini alikuwa anataka kwenda kutoa ushuhuda wa amani. Japokuwa hakuruhusiwa, hata kama alikuwa tayari kuvaa makombati ya kijeshi , kwa njia hiyo anasema tunaweza kuona shahuku hiyo ni kama vile ya Baba Mtaktifu Francisko.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.