2017-04-03 16:56:00

Husika katika mshikamano na nchi Takatifu kwa siku ya Ijumaa Kuu


Ninatoa wito wa pamoja kwa binadamu wote , kwa wakristo wote anayetuunganisha katika Kristo ili waweze kuwa na ukarimu wa kujitoa kuchangia amani katika eneo la Yesu, katika nchi Takatifu , ili nanyu mpate kuwa mstari wa mbele katika kujenga dunia hii.
Ni wito wa Kardinali Leonardo Sandri Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki ambao ameutoa  kwa waamini katika kujitoa kwaajili mchango wa Ijumaa Kuu wa  nchi Takatifu wakati kanisa linajiaandaa kwenye wiki takatifu kutokana na kwamba ni  utamaduni wa kila ijumaa takatifu kufanya hivyo.Shirika la habari la Sir limemnukuu Kardinali Sandri  akiwakumbusha umuhimu wa kuhifadhi maeneo matakatifu,na kwamba  ni mojawapo ya njia ya sala na maombi yetu sisi kwa Bwana bila hata kufika lakini  inatufanya tufike moja kwa moja kwa Mwokozi ambaye ni mwana  wa Mungu. Mbele ya matukio mengi ya kutisha yanayotokea katika nchi hiyo, ipo hatari kuyaona kwamba hayagusi sehemu kubwa ya watu na hata kukisa kuwajibika kuhusiana na suala hilo. 

Kwa njia ya kujitoa sadaka katika mchango wa Ijumaa Kuu kwa ajili ya nchi Takatifu , ni kushiriki binafsi katika kubadili hali halisi ya vita, majanga,ugaidi, nguvu na mgawanyiko; na hivyo hata wewe unahusika kuongeza mabadiliko ya nchi hiyo na wala siyo wengine. Aidha amesema tendo la kujitoa kwaajli ya amani katika maeneo ya Yesu , ambayo yameitwa kutoa mshikamano wa nchi takatifu , ulianzishwa na matashi ya Baba watakatifu kwa ajili ya kuendeleza uhusiano mkubwa uliopo kati ya wakristo wote duniani na maeneo matakatifu.Mshikamano huo kwa kawaida ufanyika siku ya Ijumaa Kuu , ni kisima cha msingi katika kuhimarisha maisha ya kawada ya kitume huko katika maeneo matakatifu,hiyo pia ni nyenzo ambayo Kanisa Katoliki limetoa wajibu wa ushirikiano kati ya jumuiya za Maknisa ya Mashariki.Miaka ya hivi karibuni Mwenyeheri Paulo VI katika  waraka wake wa kitume usemao “mipango yetu  (Nobis in Animo) uliotolewa tarehe 25 Machi 1974, ulitoa msukumo kwa ajili kuhimarisha ya nchi Takatifu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.