2017-04-01 15:33:00

Kanisa nchini Italia wafanya wiki ya matendo ya huruma


Matendo ya huruma na maombi ni uzoefu wa majiundo ya mioyo katika kujirudi na  kukutana na Mungu kwa njia ya upendo kwa ndugu  kwa kufanya matendo halisi ya huduma. Hayo ni maneno Mkurugenzi wa Caritas Jimbo Monsinyo Enrico Feroci wakati wa kuwakilisha wiki ya matendo huruma mapema  mwisho wa mwezi wa tatu. NaJumapili tarehe 2 Aprili 2017 maparokia yote nchini italia  yameandaa kufanya matendo ya huruma na wakati huo Jimbo la Roma wakijiandaa  terehe 6 Aprili 2017 kufanya mkesha wa sala na maombi yatakayo ongozwa na Kardinali Agostino Vallini, pamoja na  Frere Alois Mkuu wa Jumuiya ya sala Taize.

Kwa upande wa mji wa Roma kuna vituo 49 vya makaribisho vinavyoendeswa na Jimbo katika kujibu hali halisi ya wahitaji wa mji.Wakati huo huo mkesha wa maombi utafanyika  katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane Laterano tarehe 6 Aprili ukiongozwa na Kardinali Agostino Vallini na pia Kardinali atawakabidhi utume wa kichungaji wahamasishaji wa upendo katika kujitolea kijimbo na kijamii.Sala na maombi yataongozwa na Jumuiya ya Taize na pia Mkuu wa Jumuiya hiyo atatoa tafakari ikiwa na  mada ya “ huruma mliyopewa, ni huruma mnayopaswa kuitoa,
Taarifa zinasema kuwa makusanyo ya matendo ya huruma yatagawanywa katika vituo 49 vya jimbo, kama vile jumuiya mbali mbali zinazowapokea watu wenye shida na pia  nyumba za kijamii. Katika utume huo taarifa zinaonesha takwimu tangu mwaka 2016 kwamba watu wa kujitolea ni elfu sita na amabao wametenda kazi  bila kuchoka katika vituo mbalimbali kwa kutoa chakula zaidi ya watu 10,000 , wamepokea watu 2,400 wasio na makazi, 5,000 wagonjwa na kuwatembelea wafungwa 5,000.

 Aidha  kuna wajibu mkubwa wa vituo vya ushauri wa parokia ambapo wamewasiliza familia 48,000 .Sahani za chakula 350,000 zimetolewa , watu 200,000 wamepata mahali pa kulala, 15,000 wamepata huduma ya afya , na kuwatembelea wazee 10'000. Huduma nyingine imetolewa katika sekta ya mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya 6,000 katika shule za Roma, hawa ni pamoja na kuudhulia  mikutano , semina na mafunzo kwa ajili ya waganga na waandishi wa habari , vilevile hata katika elimu ya juu .Shukrani kwa Mungu katika zawadi ya mwaka Jubilei ya huruma 2016 ambapo matendo ya huruma yamewezesha kufanya mambo makubwa hayo. Shukrani pia kwa ziwaendee aina nyingine za mshikamano ambazo zimetokea  kwenye maparokia ya Rona , kwa mfano wa mradi wa,”nilikuwa mgeni mkanikaribisha”. Ni  jumuiya takribani 130 wamekuwa  tayari kuwapokea wakimbizi ambao Baba Mtakatifu Francisko alitoa wito wa nguvu ili jumuiya za kikiristo watawa, parokia na taasisi mbalimbali kufungua milango. 

Miaka 50 iliyopita anasema Monsinyo Enrico Feroci, kwa msukumo wa Mtaguso Mkuu wa Vatican II , Mwenyeheri Paulo VI alitoa Waraka wa Maendeleo ya watu na kazia: haki, amani, utu,na kwamba utimilifu wa mwanadamu, unaoongozwa na tunu msingi za maisha ya kiroho. Ikumbukwe ilikuwa ni tarehe 26 Machi 1967, na hivyo miaka 50 iliyopita, alipoandika Waraka wa Kitume, “Maendeleo ya watu” alikuwa anakazia maendeleo endelevu ya binadamu.Kwa njia hiyo mshikamano unatakiwa kujikita katika kanuni ya amani , ili kulinda, kudumisha na kutetea utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Monsinyo Enrico Feroci anabainisha kuwa huo Waraka ulikuwa ni wa kinabii katika nyanja ya upeo mkubwa endelevu, wenye  uwezo wa kusoma kwa kina ishara za nyakati. Kwa maana hii tukio hili ni kiini cha Kwaresima hasa kwa mtazamo wa kutoa wito juu ya  watu na njaa, na hali halisi ya mwanadamu anayezidi kuteseka;kwa mtazamo wa umasikini katika hali zote za kijamii na ukosefu wa haki, ambao umezidi kupanuka na kufikia hata miji yetu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vartican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.