2017-03-31 13:14:00

Viongozi wa dini ya Kikristo Ujermani kutoa wito wa kusaidia baa la njaa


Mamilion ya watu katika pembe ya Afrika wanakufa na njaa, ni maneno ya Kardinali Reinhard Marx Askofu Mkuu  Katoliki wa Munich na Freising  Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ujerman , na Askofu Mkuu Heinrich Bedford-Strohm Rais wa Baraza la Kanisa la  Kiinjili  wakitoa wito kwa watu wote kutoa msaada kuhusu hali ya mateso kwa watu wa pembe ya Afrika.Ukame wa muda mrefu katika mikoa na maeneo yenye kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewewe katika nchi ya Sudan ya Kusini, imesababisha matokeo mabaya haya. Hivyo maaskofu katika ujumbe wao wanasema hatuwezi kukaa na kutazama watu wakifa kwa njaa na utapia mlo, na hivyo wanaalika waamini kutoa msaada halisi wa hali na mali kwa ajili ya wenye shida na pia kuwaombea.Pamoja na hali mbaya ya njaa huko Sudan ya Kusini  pia hata nchi ya Uganda, Kenya, Somalia na Ethiopia, nchi ambzo zinaendelea na matatizo ya baa la njaa na ukame kwa kusababisha hata ukosefu wa malisho ya wanyama.

Hivi karibuni taarifa ya  Umoja wa Mataifa imesema, maisha ya watu zaidi ya milioni 20 yako hatarini kwa ajili ya baa la njaa na hasa nchi za pembe ya Afrika. Hata hivyo serikali ya Kenya na  Sudan ya Kusini walitangaza hali mbaya ya ukame kuwa ni janga la kitaifa ili kuweza kupata msaada kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa kwani kuna watu  wanaoteseka, wamekata tamaa na wengine wengi  kupoteza maisha kutokana na makali ya njaa katika maeneo mengi ya nchi hizo. Baa la njaa ni moja ya majanga ambayo yamemkumba mwanadamu kwa kipindi kirefu katika historia yake. Roho nyingi zimepotea kwa sababu ya janga hili Kwa namna hiyo Askofu Mkuu Bedford Stohm anatoa wito kwa ajili ya hao waathirika, kwamba, daima wanaoshambuliwa kwanza ni masikini kati ya masikini, wagonjwa watoto na wazee, kwa maana hiyo mateso hayo na mengine ya kibinadamu hayapaswi kupita bila kutazamwa na nchi ya Ujermani

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.