Baraza la Maaskofu wa Marekeni wakiuunga mkono Baba Mtakatifufu, wanatoa ujumbe
wa nguvu katika utetezi wa mazingira kwa ajili ya kupunguza hewa ya ukaa nchini.Ni
kwa mujibu wa ujumbe wa Baraza la Maaskofu kufuatia kiongozi wa Marekani Donald Trump
kutoa amri ya kuondolewa kwa sheria zilizokuwa zimetiwa saini na mtangulizi wake Barack
Obama kuhusu taifa hilo kuwa na nishati salama.
Ujumbe ulio tiwa sahini na Askofu Frank J.Dewane Rais wa Kamati ya Haki ya ndani na
maendeleo ya binadamu ,inatoa hali ya kudhoofisha idadi kubwa ya ulinzi wa mazingira,
na kuzima mipango ya kitaifa ambayo imekuwa na malengo ya kupunguza hewa chafu katika
kituo kikubwa cha umeme kwa asilimia 32% kufikia mwaka 2030.
Maagizo hayo ya Bwana Trump, yanaweka hatari ya malengo ya utetezi wa mazingira, bila kuchukua hatua madhubuti kwa kuhakikisha ulinzi wa mazingira na hata viumbe wanaoishi. Vilevile maaskofu wanayo hofu ya kwamba kwa bahati mbaya maamuzi ya Trump kwa ajili ya nchi hiyo, pia yanawezekana kufikia hata ngazi ya kimataifa.Ujumbe huo wa maaskofu uliotiwa saini na Askofu Dewane unasema sera zote za kisiasa zinapaswa kusimamia utekelezaji wa mazingira kwa upeo wa kiujumla na binadamu, aidha wanasema kwamba baadhi ya nchi zimeweza kupiga maendeleo ya kuweza kupunguza hewa ya ukaa, na hivyo juhudi hizi hazina budi kuhimarishwa bila kuwa na vizingiti au masharti. Mwisho wa ujumbe wao wanaeleza kile ambacho anasema Baba Mtakatifu Francisko katika wosia wake wa sifa kwa Bwana kuhusiana na ulinzi wa mazingira nyumba yetu na hivyo maaskofu wanatoa wito wa kusikiliza kilio cha nchi na cha masikini,zaidi wale wanao ishi katika mazingira magumu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |