2017-03-29 15:27:00

Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni mashuhuda wa furaha ya Injili


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Barani Ulaya kuanzia tarehe 28- 31 Machi 2017 linaadhimisha Kongamano la Vijana Barani Ulaya linaloongozwa na kauli mbiu “Kuwasindikiza vijana ili kujibu kwa uhuru kamili wito wa Kristo”. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu mkuu Juan Josè Omella Omella wa Jimbo kuu la Barcellona, Hispania, anapenda kuwasalimia na kuwatakia mema washiriki wote wa Kongamano la Vijana Barani Ulaya.

Baba Mtakatifu anapenda kuchukua nafasi hii kuwahimiza ili kutafakari pia changamoto za Uinjilishaji katika mchakato wa kuwasindikiza vijana, ili kwa njia ya majadiliano na kukutana pamoja na vijana, kama viungo hai vya familia ya Kristo, ili hatimaye, vijana waweze kutambua kwamba wao ni vyombo na mashuhuda wa furaha ya Injili katika medani mbali mbali za maisha. Baba Mtakatifu mwishoni, anawaweka vijana wote hawa chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.