2017-03-28 14:48:00

Nchi Mashariki ya Afrika IGAD kuafikiana kusaidia wakimbizi Somalia


Shirika la Kiserikali la Ustawi wa nchi za Mashariki mwa Afrika IGAD hivi karibuni limefanya mkutano wao na  kuafiki kusaidia kuwarejesha kwa hiari katika nchi yao wakimbizi wa Somalia. Katika taarifa iliyotolewa baada ya kumailizika mkutano maalumu wa viongozi wa nchi wanachama wa IGAD chini ya uenyeji wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Nairobi. Viongozi wa IGAD wameafikiana pia kuhusu kuimarisha usalama na utulivu nchini Somalia, pia wametaka uwezo wa Kikosi cha Umoja wa Afrika cha Kulinda Amani Somalia (AMISOM) uimarishwe ili kurejesha usalama katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.Halikadhalika viongozi wa IGAD wametaka nchi za eneo hilo zisaidiwe katika kuwalinda na kuwapa hifadhi wakimbizi wote sambamba na kuhakikisha wanaishi katika maisha ya kibinadamu.Katika makambi hadi sasa raia wa Somalia wapatao Milioni mbili wameyakimbia makwao huku wengi wakiishi nchini za jirani kama Kenya, Ethiopia na nchini Uganda,Yemen,Djbouti.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukitoa wito kwa nchi  hasa Kenya kuendelea kuwapa hifadhi wakimbizi wa Somalia.Aidha katika Mkutano huo naye Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dusalegn amesisitiza wanachama kuwa wakimbizi lazima wahifadhiwe kwa vyovyote vile Kulingana na sheria za kulinda wakimbizi za kimataifa.

Mkutano huo wa Nairobi ambao ulifanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn umehudhuriwa pia na marais  Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia, Yoweri Museveni wa Uganda, Salva Kiir wa Sudan Kusini, Ismaïl Omar Guelleh wa Djibouti na Makamu wa Rais wa Sudan, Hassabo Mohamed Abdulrahman.Na mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi George Okoth-Obbo (UNHCR) ametiwa moyo  kwa sababu ya uwajibikaji huo kwa ngazi ya kikanda, kuhakikisha kwamba wanajali na kuwalinda wakimbizi wa Kisomali.Na pia Shirika la Wakimbizi limesisitiza umuhimu wa kuunda hali ya kuhakikisha usalama na hali bora ya kijamii, kuanzia kwa wasomali wanaoomba msaada ndani ya nchi, pia wakimbizi wanaotaka kurudi makwao.Mkutano huo pia umeonesha kwamba kurudi siyo suala la changua au hiari bali cha msingi ni uwepo uwezekano wa mshikamano katika kuchangia na kushirikishana majukumu kimataifa kwa njia ya uwajibikaji kama vile kutafuta mbinu za wakimbizi kurudi Somalia, uwezekano wa vituo vingine kwa kusafirisha madawa,uwezekano wa uwepo wa mipango ya kibinadamu,kuunganishwa kwa familia zao, na pia kuwapa fursa wahamiaji wenye ujuzi mafunzo.

Zaidi ya watu milioni mbili ya Wasomali wamelazimika kikimbia kwa sababu ya mgogoro wa muda mrefu zaidi duniani.Inakadiriwa kuwa milioni moja ya wakimbizi wako ndani ya nchi ya Somalia, na wakimbizi, 900,000 kati yao ni wenye umri wa uzee .Wakimbizi walioko Kenya ni 324,000, Ethiopia, 241,000,Yemen 255,000, Uganda 39,500, na Djibouti 13,000. George Okoth-Obbo pia ameongeza kusema kuwa hata hivyo, ukame ni tatizo kubwa na kwamba ni lazima kupata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.Na  kwamba ni muhimu kutambua kuwa mkoa unakabiliwa na matatizo kama vile ukosefu wa usalama ukame na chakula, na kutishia kusababisha njaa na kifo. Ni takribani milioni 62 ya watu na kati yao nusu ya wakazi wa Somalia wanahitaji huduma ya kibinadamu.Kwa upande wa utapia mlo taarifa zinasema  unazidi kuongezeka kufikia watoto 944,000 wanaonesha kuwa na utapia mlo sugu.

Sr Angela Rwazaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.