2017-03-28 13:59:00

Mwanaharakati wa kutetea haki Kathy amefariki dunia


Afrika Kusini inaomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi na aliyekuwa mfungwa wa kisiasa Ahmed Mohamed Kathrada. Alijulikana  kwa jina maarufu kama Kathy, mwanaharakati huyo amefariki dunia akiwa na miaka 87 baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Johannesburg. Akiwa na miaka 17 kuanzia miaka ya 1950, Kathrada aliondoka shuleni na kuanza kujihusisha na maswala ya uanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na kupigania haki. Msimamo wake ulisababisha uongozi wa Afrika Kusini wakati huo kumpa kifungo cha maisha jela katika Gereza la Kisiwa cha Robben mwaka 1964 kwa kujihusisha na kundi la Umkhonto we Sizwe vuguvugu la kupigania haki. 

Katika kifungo hicho akapata fursa ya kukutana na wafungwa wengine kama vile  baba yetu Nelson Mandela, Walter Sisulu, Govan Mbeki, Andrew Mlangeni, Billy Nair, Elias Motsoaledi, na Raymond Mhlaba. Alitumika kifungo  kwa miaka 26 na mwaka mwaka 1990 akaachiliwa huru na kuchaguliwa kuwa Mbunge kupitia chama chake cha ANC.Kipindi chote cha uhai wake ameandika kitabu kuhusu maisha yake na kile alichopitia Gerezani katika harakati za kulikomboa taifa la Afrika Kusini.Wengi wanakumbuka kitabu chake kinachofahamika kwa jina No Bread for Mandela- Memoirs of Ahmed Kathrada.Pamoja na viongozi wengi wa kutetezi wa haki za watu  nchini Afrika pia katika maisha yake amewahi kuwa pia mshauri wa kiongozi wa kwanza mweusi mwasisi wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye alifariki dunia mwaka 2013.Harakati zake za kutete nchi yake hazikuishi hapo kwani miaka ya hivi karibuni amekuwa akikosoa uongozi wa serikali pamoja na chama cha ANC.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.