Ziara ya Baba Mtakatifu katika Gereza la Mtakatifu Vottore ilikuwa ni moja ya ziara
yenye msisimko wakati anaelekeza safari yake Milan. Amewashukuru kwa makaribisho yao
na kusema anajisikia kuwa mmoja kati yao.Maneno hayo ameyatamka kwanza kwa wafungwa
walio mpokea kwa shangwe kubwa na kuwasalimia kila mmoja kwa mkono na kuongea nao
kwa maneno mepesi kabisa kabla ya kwenda kula chakula cha mchana ndani ya Magereza.
Mwandishi wa Radio Vatican, alipata habari zaidi kuhusiana na makaribisho ya Baba
Mtakatifu kutoka kwa Padre anayehudumia Kanisa dogo la magereza hiyo.Amesema umekuwa
muda mzuri sana na wenye maana kwasababu Baba Mtakatifu amefanya uchaguzi wa ajabu,
yeye binafsi amewasalimia watu zaidi ya 850 wakiwemo hata maaskari.Yeye binafsi amewapitia
na kutoa mkono wake, au akitoa neno lake wakati huo huo akipita kumetokea aina fulani
ya kimya kana kwamba utafikiri ni sala ndani ya Kanisa, wakati yeye kwa mwendo taratibu
anawasalimia.
Kuhusu uzoefu na hisia za maneno ya Baba Mtakatifu Padre anasema , Baba Mtakatifu Francisko amesema hawali ya yote hatupaswi kusema kwamba hawa wanastahili kwasababu kwamba sisi hatujuhi historia ya mtu fulani,au hutujuhi kilichopo nyuma yake.Yote hayo tunapaswa kumwachia Mungu aliye hakimu, tunachopaswa kufanya sisi ni kutazama dhambi zetu,na taabu zetu. Baadaye Baba Mtakatifu amegusia juu ya Injili ya Mtakatifu Matayo isemayo "ni wakati gani nilikuona gerezani, kwa namna hiyo akaongeza ;“ninyi kwangu ni Yesu”.Aidha Baba Mtakatifu Franciko amesema juu ya mitazamo yao,kwamba inapaswa kuona upeo wa mkubwa , kwasababu baadaya ya gereza kuna upeo mkubwa wa maisha na matumaini.
Baada ya makutano hayo Padre anasema, mmoja wa wafungwa wakati wanarudi , amemwambia kuwa, kwa masaa mawili yamepita utafikiri siyo mfungwa gerezani. Padre anasema kwa namna hiyo ni kama vile amewapatia uhuru wa ajabu katika makutano hayo.Wengi wao walikuwa na furaha kubwa hadi wengine kuoneshaa machozi .Kwa maana hiyo unaweza kufikiria kama kwamba Baba Mtakatifu amefungua milango ya gereza, kwasababu wote tulikuwa pale waume kwa wanawake mbele ya Baba ambaye ametoa matumaini na nguvu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |