2017-03-26 10:31:00

Mtindo wako katika kiti cha Petro ni ushuhuda na ishara hai kwetu!


Mara baada ya ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa Monza, Kardinali Angelo Scola Askofu Mkuu wa Jimbo Kuuu la Milan ametoa maneno ya kumshukuru Baba Mtakatifu Francisko akisema,baada ya maadhimisho ya ekaristi takatifu katika eneo hili, ambalo limegeuka  kuwa Kanisa Kuu chini ya hanga iliyofunguka;na kabla ya kuingia katika uwanja wa mchezo wa Mpira wa Mtakatifu Siro, mahali ambapo  Vijana waliopata kipaimara mwaka huu wanakusubiri, ninatoa asante. Asante hiyo ni kwa niaba ya Kanisa la Ambros na kwa ajili ya watu wote wa Mkoa wa Lombardia kwa siku ya leo ambayo umependa kukaa nasi. Ni siku ambayo bado haijamalizika lakini iliyo jaa neema. Watu wote leo hii tumefanya uzoefu kwa mara nyingine tena katika ukweli wa maneno ya Baba yetu Ambrosi (Ambrosius) akisema: “mahali ambapo yupo Petro pale kuna Kanisa. Mahali ambapo kuna Kanisa pale hakuna kifo, bali yapo maisha ya milele”.

Ishara ulizo tenda zina maana kubwa na ni maelekezo ya kuinjilisha katika jimbo letu hili kubwa. Kwa namna ya pekeke kuwapa mkono masikini , wahamiaji , na wafungwa ni kutuelekeza njia ya kufuata. Hiyo ni kwa sababu Yesu aweze kuwafikia wote, mama Yesu  ni amani yetu,ni wema,ni ukweli,ni haki ambayo kila mtu katika nchi yetu anahitaji,na anatakiwa kila yeyote anayeishi aweze kuguswa katika mioyo.Masikini wanayo mambo mengi ya kutufundisha,kwani katika injili ya furaha inasema kwa kushiriki mateso ya waamini,ni kuongezeka mateso ya Yesu mwenyewe. Mtazamo wao na wenye uchungu lakini mwepesi unaangaza na kupanua mtazamo wetu japokuwa mara nyingi tupo mbali na mtazamo wao.

Tangu mwanzo wa utume wako, mtindo wako wa kichungaji katika utumishi wa Petro umekuwa ni kielelezo cha ushuhuda mmoja na ishara ya mifano halisi,utamaduni na mafundisho. Kwa njia ya ushuhuda huo, tunataka kujifunza kuanzia shukrani kwa namna ya furaha na uhamasishaji wako unaojieleza katika siku ya keo.Na kama usivyo acha kuomba, hata sisi tunakuhakikishia sala zetu za kila siku kwa mama yetu Maria.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.