2017-03-25 17:46:00

Yesu mwingi wa huruma anachana taabu zetu,na kukutana nasi!


Baba Mtakatifu , Kanisa Kuu ni moyo wa maisha ya Kanisa na sehemu ya kimbilio la watu wote wa Milano wakiwemo makuhani, watawa, kike na kiume na wengine wenye wakfu katika karama za utume wao kwenye Kanisa la Mtakatifu Ambrosio na Mtakatifu Charles. Idadi kubwa kati yao wanafuatia tukio hili katika uwanja mkubwa wa Kanisa na pia katika majumba yao.Tunayo shahuku kuwa ya kukusikiliza na tunakushukuru kwa kuchangua aina hii ya mazunguzo. Ni maneno ya utangulizi wa salam za kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko katika Jimbo Kuu la Milano, kutoka kwa Kardinali Angelo Scola kabla ya kuanza mkutano na mapandre na watawa kwenye Kanisa Kuu la Milano.

Sehemu ya waraka wa Injili ya Furaha inasema jambo zuri ambalo liko ndani ya moyo wetu yaani “habari njema inasisitiza jambo la muhimu,yaani kile ambacho ni chema , kikubwa na kinavutia na wakati huo huo ni muhimu,(EG 35).Kama ulivyo kuwa umeeleza huko kwenye Mkutano wa Firenze ya kwamba tunaishi nyakati za mabadiliko, zaidi ya nyakati zilizopita.Mabadiliko tunayoishi siyo sababu ya kukata tamaa bali ni ya kuongoka watu binafsi na katika jumuiya zetu na hasa ile hali ya kutoka nje kwa ajili ya kukutana na watu, ambayo ni ishara ya huruma inayotuliza na kutoa amani.
Yesu aliyejaa huruma , anachana chana taabu zetu. Yeye ni shuhuda mwaminifu, haachi kamwe kutupatia mkono wake na kukutana na sisi.Anamalizia Kardinali Scola akisema ;Kama vile maneno ya Mtakatifu Charles Borromeo aliyo mwambia Mtakatifu Pio wa V, nasi tunarudia kusema kwamba “hata sisi tunakuhakikishia sala zetu, ili Mungu aweze kukujalia utakatifu ambao hata sisi tunaweza kuuona kwa nyakati zetu , katika maendeleo ya kiroho ya Kanisa na ambalo Ulimwengui wa sasa una kiu na kusubiri huruma ,ili upate kuwa na ari ya utume wa utakatifu wenu.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.