2017-03-21 15:50:00

Kusamehe ni fumbo gumu inahitaji sala,kutubu na kuona aibu!


Kusamehewa na kusamehe ni fumbo lenye ugumu  wa kulitambua, inahitaji sala na kutubu pia kuwa na aibu. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa misa ya asubuhi Jumanne 21 Machi 2017 kwenye misa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican. Baba Mtakatifu ameongelea juu ya umuhimu wa kuwa na utambuzi wa maajabu ya Mungu anayo tujalia katika  huruma yake na ili tuweze kuitenda huruma hiyo hata kwa wengine,  pia ameonya kuacha  tabia ya unafiki, hadi kufikia kuiba msamaha usio stahili katika maungamo.
Anasema msamaha ni fumbo ambalo ni vigumu kutambua.Hayo anayasema kutokana na Neno la Mungu kuhusu mfano wa mtumishi asiyesamehe baba Mtakatifu Francisko anaelezea juu ya tendo la huruma kama ilivyo jieleza kutoka  Injili ya Matayo (Mt 18,21-35)
Anachambua Injili ya siku akisema hatua ya kwanza ni aibu ya dhambi binafsi , ni neema ambayo sisi binafsi hatuwezi kuipokea.Ina uwezo wa kujikita katika watu wa Mungu na kufanya uzoefu wa huzuni,kujisikia kudhalilika, na kujisikia wenye dhambi, kama vile somo la kwanza la  Nabii Daniel na sala yake, tofauti na Injili,kwani katika Injili ya siku, wahusika wanashindwa kusali. Bwana wake alimsamehe mtumishi pamoja na kuwa alikuwa na madeni makubwa, lakini pamoja na kupokea msamaha huo, yeye binafsi hakuwa na uwezo wa kusamehe wengine wenye madeni. Hiyo ni kwasababu hakutamba fumbo la msamaha, anasema Baba Mtakatifu Francisko.

Baba Mtakatifu anajaribu kutoa mifano halisi,akisema Je nikiwauliza , je ninyi nyote ni wadhambi?mtajibu ndiyo baba wote, je ni bi namna gani ya kupata msamaha wa dhambi?.mnajibu ,tunaungama, je ni kwa jinsi gani unakwenda kuungama?, jibu, mimi ninakwenda na kuungama dhambi, na Padei ananisamehe, na pia kunipatia malizi ya kusali salama Maria mara tatu na baadaye nenda kwa amani.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema, wewe hujambua,! Kwa sababu umekwenda  kuungama kama vile kufanya mchakato wa bank , au kufanya kufanya shughuli za kiofisi.Wewe hukwenda ukiwa na aibu kwa kile ulichotenda.Bali wewe umeona baadhi ya madoa katika nafsi yako, na umekosea kwasababu umeamini ya kwamba katika maungamo utafikiri ipo  jiki ya kuweza kutoa madoa hayo. hukuwa na uweze kwanza wa kujisikia aibu kwa ajili ya dhambi zako.

Anasema katika chumba cha maungamo usiibe msamaha wa usio wa kweli bali unapaswa kuwa na ufahamu wa uhuruma ya Mungu. Kwa maana msamaha utokao kwa Mungu , yaani maajabu aliyokutendea katika moyo wako, ni lazima uingie katika nafsi , badala yake ukitoka humo na kukutana na rafiki ukaana masengenyo kwa wengine , ni kuendelea kutenda dahambi. Na ndiyo maana ya kwamba mimi ninaweza kusamehe iwapo mimi ninajisikia kusamehewa.Kama nafsini mwako hujisikii kusamehewa, haitawezekana kamwe kusamehe. Daima kuna hali ya kutaka kupambana na wengine, lakini msamaha ni wa jumla.Kwa njia hiyo ninaweza kufanya hivyo iwapo kweli ndani ya nafsi yangu ninajisikia aibu, kwa njia ya aibu nina lazimika   kuomba msamaha kwa Mungu. Nikijisikia kusamehewa na Baba nami ninaweza kusamehe. Anasisitiza Baba Mtakatifu , kama siyo hivyo, siyo rahisi na hatuna uwezo wa kusamehe kabisa , na ndiyo maana tendo la msamaha ni fumbo.

Mtumishi katika Injili ya siku,alifikiri atakuwa mjanja ,na kukosa kutambua ukarimu wa Bwana wake.Je ni mara ngapi unatoka chumba cha maungamo,ukiwa na mawazo kama hayo ya kwamba umepokea msamaha kama wa mtumishi huyo?,lakini hiyo siyo njia ya kupokea msamaha bali ni unafiki wa kuina msamaha , msamaha usio wa kweli.Baba Mtakatifu anamalizia , Tuombe Bwana leo hii atupatie neema ya kutambua nini maana ya sabini mara saba.Tuombe neema ya kuona aibu mbele ya Mungu. Hiyo ni neema kubwa, na ya kuona aibu mbele ya dhambi ambapo tunaweza kupokea msamaha na neema ya ukarimu kwa ajili ya wengine , kama Mungu amenisamehe dhambi zangu nyingi je mimi ni nani nisiweze kusamehe?

 








All the contents on this site are copyrighted ©.