2017-03-18 15:56:00

Baraza la Maaskofu Italia kutoa msaada wa fedha Sudan ya Kusini


Baraza la maaskofu nchini Italia , wametoa msaada wa euro milioni moja kwa aajili ya kununua mahitaji ya wakimbizi na wathirikia wa migogoro kwa miaka mingi wako katika umwagaji wa damu huko Kusini Sudan. Kiasi hicho ni kupitia ofisi ya Caritas  Italia , itasaidia katika huduma za afya na lishe, katika  mahospitali ya Madaktari na Afrika (CUAM) na Hospitali ya Shirika la Wakomboni huko Wau na pia kwa miradi mingine ya jamii na kiuchumi hasa kwa upande wa Caritas mahalia. Caritas ya Italia itawajibika katika kufuatilia huduma hiyo kwa ajili ya watu wanaozidi kuteseka. 
Takwimu za umoja wa mataifa zimeonesha , karibia watu 100,000 wana hatari ya kifo cha njaa , wakati watu milioni tano na nusu wanaonesha kuwa katika hali hiyo ya ukosefu wa chakula kufikia mwisho wa mwaka huu.Ni karibia watu milioni mbili wamekimbia vita na wanahitaji msaada wa hali na mali kwa ajili ya mahitaji .

Hata hivyo hata Madaktari na Afrika (CUAMM) wametoa wito kwa ajili ya kusaidia nchi hiyo ,wanasema Sudan ya kusini ni mojawapo ya nchi ya Afrika inayo hitaji msaada wa kibinadamu; yamedhibitishwa na Padre Dante Carraro Mkurugenzi wa Madaktari na Afrika , CUAMM Shirika lisilo la kiserikali , linalotenda wajibu wake  katika ngazi ya afya. Anasema bei ya unga na mchele ni zaidi ya kima cha chini cha mshahara. Sarafu ya nchi haina thamani kwa sasababu ya kushuka bei ya mafuta, wakati huohuo nchi hiyo ni yenye utajiri wa petrolina .Halikadhalika katika maeneo mengine ya nchi kuna ugonjwa wa kipindupindu.

Baada ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, Cuamm leo hii inajikita katika makambi ya wakimbizi huko Suda ya kusini .Wapo wahudumu 1023 mahalia na 53 wa Kimataifa, kati yao 20 ni wataliani lakini idadi ni ndogo kulinganisha na huduma na mahitaji ya wengi.Padre Carraro anasema kila siku usiku kuna mabomu ambapo watu mijini hawawezi kuthubutu kutoka nje.Serikali zote mbili zimeshindwa kupata mwafaka katika mazungumzo, wakati huo kila sehemu ni kuishi kwa hofu maana wanajeshi wanazuia mawasiliano, ka mfano namna ya kusafirisha chakula katika baadhi ya vijiji.Anaongeza, kila siku Padre huyo madaktari na wahudumu, wanaona familia zinavyo angaika kwa ajili ya watoto, maana hawana chakula cha kuwapatia watoto wao.Ni kutazama kifo machoni!.Vituo vya hospitali zao vimejaa watu wengi amabapo wanaweza kupata chakula na mablanketi ya kuwafunika.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.