Jumuiya za kikristo zinapaswa kutambua kwamba maeneo ni salama ambapo waathirika
wa unyanyasaji wa majumbani wanapaswa kuchukuliwa kwa makini, kuaminiwa na kuheshimiwa
. Na kwa wale walio husika na ukiukwaji wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuoneshwa
wazi matendo yao.Hiyo ndiyo ufupisho wa lengo la hati mpya ya Kanisa la Uingereza
ambayo imerudia upya kutazama jambo hilo , kwani ilikuwa tayari imechapishwa mwaka
2006.
Mashambulizi na kusumbuliwa ndani ya nyumba , itakuwa ni moja ya mada katika semina
na majadiliano ya kina , semina ya maandalizi na mikutano ya makundi ya vijana.Wale
wanao husika na kukabiliana na unyanyasaji wa majumbani ndani ya Kanisa la Uingereza
wanalazimika pia kushirikiana na wawakilishi wa Serikali ya Uingereza inayojikita
katika uwanja huu na pia sekta mbalimbali za vyama.
Mkutano wa Maaskofu wa Kianglikani ,katika waraka mpya wameomba kwamba wafanyakazi
na kujitolea ambao wanafanya kazi karibu na watoto, vijana na watu wazima wenye kuishi
katika mazingira magumu , kufanya mafunzo maalumu na maandalizi ambayo yatawawezesha
kukabiliana kwa kina zaidi katika kutafuta haki ya wale wanao nyanyasika majumbani
, na kuwatambua wahusika pia kupata kuwasaidia waathirika.
Waraka huo wa pili umetolewa na maaskofu wa kianglikani nchini Uingereza wenye mada
ya “kuhamasisha usalama zaidi wa Kanisa, unawaajibisha maaskofu mapadri, mashemasi,
wasomaji neno la Mungu, walei na kila mtu binafsi anaye jibidisha katika hali hii
ya Kanisa kuheshimu mwongozo wa kanuni katika suala hili la manyanyaso ya majumbani.Askofu
wa kuanglikan wa Bath na Well Peter Hancock, kwa miaka mingi yuko mstari wa mbele
katika kulinda waathirika anasema , Kanisa la Uingereza linajibidisha kusimamia wale
walio athirika na wale na mbao kwa sasa wakao katika mchakato huo.
Askofu anakumbusha kwamba manyanyaso ya kila aina ni kinyume na mapenzi ya Mungu na
ni ukiukwaji wa utu wa mwanadamu.Kila mmoja napaswa kuwa sehemu ya kuzuia au kusimamisha
matukio hayo, pia Kanisa la Uingereza linaonesha wajibu wake kwa nguvu kusimamia kila
aina ya manyanyaso.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |