Hivi karibuni Askofu mkuu Bernadito Auza mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa alitoa hotuba katika ukumbi wa Seton wa Chuo Kikuu huko New Jersey Marekani kuhusu diplomasia ya Baba Mtakatifu Francisko,na amefurahishwa kuona anawahutubia ikiwa kama mojawapo ya matendo ya Juma la kwanza la kwaresima katika Ukumbi huo wa Chuo Kikuu na kumushukuru Profesa Bartoli kwa kumpatia fursa hii kuzungumzia na wanajumuiya ya Seton kuhusu Diplomasia ya Baba Mtakatifu Francisko, mada ambayo anasema huenda ikawa sawa katika moyo wa utambulisho Katoliki katika Ukumbi wa Seton.Katika historia ya Kanisa,anasema, hatuzungumzi historia ya kuvunjika au kuanza upya,ni kuongea mwendelezo unao wezekana wa safari ya umilele inayoongozwa na mafundisho ya kudumu kwa mantiki ya mazingira ya dunia inayobadilika.Anapenda kutoa mfano wa mashua thabiti ya Mtakatifu Petro kwamba, japokuwa inaonekana kuelea huku ikiyumbishwa na mawimbi makali.Hiyo ndiyo njia anayopenda kufikiria kuhusu diplomasia ya Vatican, kati ya Baba Mtakatifu Francisco na watangulizi wake,kwasababu hakuna mpasuko bali mwendelezo.
Diplomasia ya Vatican ni utume wa kazi ya kutenda katika dunia iliyomezwa na malimwengu,
Kanisa na kwa jina la Kanisa.Kama Kanuni na utume wake inatenda chini ya misingi
na Kanuni zake "wokovu wa roho ndiyo sheria kuu ya Kanisa.Inawezekana kutimiza kanuni
hiyo tu kama inatambua jinsi ya kunyambulisha ishara za nyakati na kuzitafsiri katika
mwanga wa Kristo, namna ya utambuzi huo na kutenda ipasavyo". (mwanga wa mataifa
4).
Ana amini kwamba ni kweli hasa katika mazingira ya uwepo wa Vatican katika Umoja wa
Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa. Lengo kuu kwa ujumla la uwepo wa mwakilishi
wa kudumu wa Vatican katika umoja wa Mataifa ,daima umekuwa ni kuleta chachu ya
Injili na Kanisa kwenye milenia nyingi ya uzoefu wa binadamu na ukweli katika utata
wa mahusiano ya kimataifa na katika mijadalaya kimataifa kuhusu matatizo yayo ikabili
dunia yetu.
Wengi wanauliza kwanini Vatican inataka kuwapo katika umoja wa mataifa.Je sasa
siyo mojawapo ya Umoja wa mataifa ,kama Rais mmoja hivi karibuni amesema ni kama club
kwa ajili ya kuwa pamoja kuongea na kuwa na muda mzuri. Alihitimisha akisema hii ni
mbaya sana.!
Lakini Askofu Mkuu Auza anasema, anaamini kwamba kuwa pamoja na kuzungumza na kuwa
na wakati mzuri , siyo jambo la kusikitishana wala baya sana , bali katika Umoja wa
Mataifa hakuna huzuni akitoa mfano wa mfululizo wa mashairi ya kale ya wimbo wa
Dan Fogelberg ukisema “ hatuna isemayo “zaidi ya hapo tumekuwa samaki katika bahari,”
na “tumekuwa nyota ya juu katika mbingu” , na “mbaya kama wao hawana nguvu zaidi kuliko
mlima mkuu “,na “mbaya zaidi bado kama wao siyo” ,”ni kweli zaidi ya mti wowote uliowahi
kukua,” kuingia ndani kuliko msitu unao anza kuota”.(Taz “Longer na Dan Forgelberg).
Hata hivyo, kwa nini, kweli, Vatican inashiriki kikamilifu sasa katika Umoja wa
Mataifa?.Umoja wa Mataifa, kama mnavyojua vizuri, ulizaliwa kwenye masalia ya Vita
Kuu ya Pili ya dunia mwaka 1945. Nchi 51 wanachama walisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa
huko San Francisco mwaka1945.
Lakini hakika Vatican haikuwa hakika upendeleo kwa mara kwanza .Mara baada ya kuanzishwa
Umoja wa Mtaifa , Vatican kwa kiasi fulani ilikuwa na tahadhali kuhusu hilo.Ilitambua
haja ya haraka kwa ajili ya mashirika ya kimataifa ya kwamba wangeweza kufanikiwa
katika shirikikisho la Mataifa,lakini ilikuwa bado na wasiwasi kadhaa .Wasiwasi ulikuwa
kwamba Mkataba wa Umoja wa Mataifa, huku wakitambua usawa wa nchi, hawakutoa kanuni
hii, tangu wanachama 5 wa kudumu wa Baraza la Usalama,jambo jingine ni kwamba siyo
wanachama wote walishiriki wa nchi nyingine kwa mfano hasa nchi zile ndogo zilizokuwa
zimepata uhuru dhidi ya wakoloni,nchi hizo zilikuwa zimetengwa.Suala jingine ni kwamba
walijadili matatizo lakini hayakuweza kutatuliwa hadi kufikia mwaka 1953, Papa Pius
XII aliuliza hadharani: "Je, katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeundwa kwa ajili
ya kuweka Mikataba tu na kwamba kamwe hawezi kuweka katika vitendo?.
Ingawa Vatican haikuwa mojawapo ya sehemu ya Umoja wa Mataifa kwa siku za mwanzo, mara nyingi walishiriki katika kazi rasmi na isiyo rasmi ya Umoja wa Mataifa lakini kwa kupewa mwaliko. Hatima Aprili 1964 Vatican ikawa na mwakilishi wa kudumu wa kwenye Umoja wa Mataifa na kuanza utume wake huko New York.Hii ilikuwa inafaa na siyo kwasababu ya kujihusisha kwa haraka Vatican katika maamuzi ya Umoja wa Mataifa , bali zaidi ya yote ni kwasababu ya nguzo ya nne ya Umoja wa mataifa ilivyowekwa katika Mkataba wake na kujieleza vizuri sana ,kwani ni nguzo nne kuu ya mafundisho katoliki ya kijamii isemayo kuzuia vita na kuhamasisha amani, ulinzi na nafasi ya utu wa mwanadamu na haki; maendeleo ya binadamu;na kusaidia mataifa katika kutoa kutoa maoni yao na kuheshimu mikataba ya kimataifa na sheria.Katika kipindi cha miaka 53 ya uwepo wa Vatican katika Umoja wa Mataifa huko New York,mara tano mapapa wamefanya ziara katika ofisi za Umoja wa Mataifa; Mwenye Heri Paulo VI Oktoba 1965, MtakatifuYohane Paulo II mwaka 1979 na 1995, Papa Benedikto XVI mwaka 2008, na Papa Francis 2015. katika ziara hizi, mapapa walionyesha heshima kwa taasisi hiyo ambayo wanaichukulia kuma chombo muhimu kwa ajili ya dunia.Kila Baba Mtakatifu aliyefika katika ofisi hiyo aliweza kutoa hotuba na kuacha ujumbe muhimu kwa ajili ya tafakari binafsi na hata kwa ngazi ya kimataifa kwa pamoja.
Askofu Mkuu Auza anandelea, hadi hapo ameendelea kuelezea juu ya diplomasia ya Vatican katika ngazi ya kimataifa na hasa katika Umoja wa Mataifa Katika ngazi ya nchi na nchi, leo hii Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 182 kati ya 193 katika dunia na nyingine ziko katika orodha ya maandalizi. Wapo mabalozi wa kitume 116 wa kudumu katika utume duniani kote wanao wakilisha Vatican katika mtandao wa kina kidiplomasia. Na kama tunavyofikiria maaskofu wetu, na makleri , watawa wanaume na wanawake , makatekista na walei anatoa mfano akiwaeleza wanafunzi kwamba ni sawa vitengo vya ujasusi nchini Marekani au pia vya nchini Urusi kwani hakuna mtu awezaye kupambana nasi katika ukusanyaji wa taarifa na shughuli kwa ngazi ya chini.Askofu Mkuu Auza anatoa mfano halisi wa historia binafsi juu ya kupata habari hizo kutoka sehemu ambazo siyo rahisi kuzipata, akisema kwa upande wa Kanisa ni rahisi kwasababu ya uwepo wa wamisionari wengi katika kila kona ya maeneo ya dunia ambayo kwa mtazamo rahisi siyo vyepesi kupata habari hizo. Kutokana na vikwazo vya muda, ni lazima sasa kuanza sehemu ya pili ya majadiliano, yaani, vipaumbele vya dipolmasia ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba,katika utumishi wake lazima kutenda kwa kina zaidi.
Kabla ya kutaja masuala maalum ambayo wao wanapaswa kuyatekeleza katika nchi moja
na katika ngazi ya kimataifa ,anaonesha hawali ya yote dhana ya kukutana na mazungumzo.Ni
tunu na dhahabu inayofunga mahusiano pamoja na meneno na matendo ya Baba Mtakatifu.Ule
msukumu una maana kuu siyo tu kwa ajili ya shughuli za kichungaji na kiroho kwa Kanisa,
bali hata juu ya masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa nyakati zetu.
Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza juu ya masuala ya "utamaduni wa kukutana , mshikamano
na upendo". Kila asemapo kuhusu masuala ya kijamii na kuhusu maswali pamoja na athari
kubwa ya kisiasa, yeye daima anathibitisha diplomasia ya kukutana kuongoza ili kuelekea
maarifa bora ya kuheshimu na kuheshimiana. Ni diplomasia ya mazungumzo katika kutatua
migogoro, kuhamasisha umoja na kupambana na tabia za kubagua. Ndiyo inaitwa safari
ya pamoja ni kama njia ya maisha. Hii ndiyo diplomasia kwamba fursa zaidi na heshima
kwa nchi zilizo dhaifu, Kanuni na sheria juu ya sheria ya nguvu, uaminifu na mahusiano
mazuri miongoni mwa mataifa na watu zaidi ya tuhuma kwa pande zote. utamaduni wa kukutana
hauwezi kupatikana kwa kujenga kuta na kukuza upweke, bali ni kwa njia ya madaraja
na milango wazi.
Askofu Mkuu Auza anawaeleza wanafunzi jinsi isivyo rahisi kueleza tafakari zote za Baba Mtakatifu Francisko kwasababu ya kutokutaka kuwaibia muda wao wa utafiti na wa kufanya kazi katika majumba yao ,lakini masuala ambayo Baba Mtakatifu anapendekeza kwa diplomasia ya mazungumzo, ujenzi wa madaraja na kukutana ni masuala ya kijamii pamoja na athari za nguvu ya kisiasa. Watu wanauliza,kwa nini Kanisa, kwa nini Baba Mtakatifu anajali kuhusu masuala yenye utata ya kijamii na kisiasa? jibu fupi kwa sababu Yesu anajali! na kama Yesu anajali, Baba Mtakatifu na Kanisa hawawezi kutokujali pia.Aidha anasema ,wengi wenu mnajua moyo wa sherehe za ufunguzi wa kifungu cha Mtaguso wa Vaticani wa Pili kuhusu masuala ya kichungaji kwa Kanisa katika waraka wa “Kanisa katika Ulimwengu Mamboleo” (Gaudium et Spes): "furaha na matumaini, masikitiko na shughuli za watu wakati huu, hasa wale ambao ni masikini au kwa njia yoyote wanateswa ndiyo furaha na matumaini, masikitiko na shughuli za wafuasi wa Kristo. Hakika, hakuna kitu cha dhati ya binadamu kushindwa kuongeza sauti katika nyoyo zao.
"Kwa njia hiyo Kutokana na maneno na matendo juu ya maswali makubwa na changamoto zinazotukabili dunia ya leo , Baba Mtakatifu Francisko anatualika kufanya hivyo ili sisi wenyewe tupate kujivika furaha na huzuni wa dunia hii, ili tupate kuchafua mikono yetu, kuwa na harufu ya kondoo , kwa kutoa huduma katika mahospitali, kujihusisha katika kukuza na kutekeleza diplomasia ya mazungumzo na kukutana,Hii ndiyo roho inayo hamasisha Vatican kuwapo katika Umoja wa Mataifa na katika mahusiano baina nchi zote duniani.Inatembea kimya bila kusema lolota wakati huo huo ikitoa ushuhuda wa pekee wa Vatican na Kanisa katika umahiri,kwani kuna haja ya kuepuka kujitambulisha kwa njia yoyote kisiasa au kiitikadii na hivyo kulinda utambulisho wetu wa kipekee na ushawishi Kitaifa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |