2017-03-16 15:42:00

2017:Vijana wa Asia kuiishi Injili katika jamii ya tamaduni tofauti


Kuwatia moyo na kuwasindikiza vijana wa Bara la Asia ili waweze kuishi na kuhamasisha utamaduni wa mshikamano na  kukutana na wengine katika jamii yenye tamaduni na  madhehebu mengi barani Asia.Hiyo ni kwasababu ya  kuchukua hatua ya kina kwa utumbuzi wa mchango wa Kanisa unao utoa katika jamii.Hilo ndilo lengo kuu la adhimisho la Siku ya 7 ya Vijana Barani Asia kwa mwaka 2017adhimisho litakalofanyika huko Jakarta nchini Indonesia kuanzia tarehe 30 Julai hadi 9 Agosti 2017. Mada iliyo chaguliwa katika tukio hilo ambayo  itashirikisha maelefu ya vijana Katoliki kutoka nchi 29 Barani Asia ni “Vijana wa Asia kwenye Sikukuu ya kuishi Injili katika jamii ya  tamaduni tofuati”. Askofu Mkuu wa Jakarta Ignatius Suharyo amewakilisha habari hizo katika vyombo vya Habari vya Fides akisema "anawaalika  vijana wote katoliki wa Indonesia  na katika nchi nyingine Barani Asia , waweze kuudhulia na kushirikishwa na roho ya mada kuu katika kutambua kuishi na umuhimu wa kuishi katika umoja kati ya utofauti.

Askofu mkuu anaeleza kuwa siku ya Vijana Barani Asia itakuwa imegawanyika katika sehemu tatu, sehemu ya kwanza itaanzia katika jimbo,ya pili, vijana watakwenda katika miji kwenye vituo vikuu, na ya  tatu itakuwa mikutano ya wahusika wa utume wa  kichungaji kwa vijana .Washiriki wote  wa siku ya vijana watakuwa wamegawanywa katika majimbo 11 nchini Indonesia ambapo wataweza kuishi uzoefu maalumu wa kushirikishana .Baadaye wote watahamia Jakarta na kufanya uzoefu wa katekesi, liturjia, sikukuu na kushirikishana kwa pamoja historia mbalimbali ya maisha yao binafsi, kulingana na mahali vijana wanapotokea katika kutafuta kilelelezo cha pamoja kinacho waunganisha katika imani ya Kristo.

Mkutano wa viongozi wa utume kichungaji kwa vijana ni fursa maalumu  ya mafunzo kwa wote watakao sindikiza vijana watakao shiriki katika siku ya vijana huko Jakarta.Hali kadhalika Askofu Mkuu anasema ili kuweza kuwashirikisha wakazi wote wa Indonesia katika utambuzi wa  siku ya Vijana kwa mwaka 2017 , wameandaa utangulizi wa azimo la mashindano ya michezo litakalo fanyika tarehe 7 Mei 2017 na washiriki karibia 5,000 watashriki.
Tukio hilo tayari limefunguliwa katika mitandao ya kijamii ambapo ni rahisi kupata habari zaidi kuhusiana na tukio hili.(www.asianyouthday.org; Facebook: asianyouthday; Twitter: AYD2017; Instagram: asianyouthday2017).

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.