2017-03-15 15:26:00

Ni zaidi ya milioni 1,5 ya watu wakimbizi kutoka Sudan ya Kusini


Shirika la saidia watoto (Save children) linasema ni zaidi ya Milion 1,5 ya watu kutoka Kusini mwa Sudan walio kimbia nchi zao kutokana na migogoro Miongoni mwao  ni watoto, wanawake wanashambuliwa na makundi ya kigaidi na kuwatesa isivyoelezeka.Mwaka 2016 walio kimbilia nchi ya Uganda kutoka Kusini mwa Sudan ilikuwa idadi kuwa zaidi ya ile iliyokatisha  bahari ya Meditranea kwa nyakati sawa za mwaka.
Kabla ya kutangaza ripoti ya Umoja wa mataifa inayo onesha masula ya  Sudan ya Kusini, upo mchakato wa mfumo wa minajili  ya makabilia yao  na njaa vilivyosabishwa maelfu ya watu kukimbilia nchi ya Uganda.Shirika la saidia watoto (Save children) ambalo tangu mwaka 1919 limejihusisha na masuala ya watoto walioko hatarini , na kuhamasisha haki , wanaripoti kuwa zaidi ya  milioni ya wakimbizi walio kimbia kutoka Sudan ya Kusini ni kutokana na mapigano ya kutisha  tangu Julai 2016, wakitafuta msaada huko nchini Uganda. Na tangu desemba 2013 ni asilimia 86% ikiwa ni wanawake na watoto .Hawa wanafika  makambini wakiwa na hofu kubwa, watoto wengine hawana msindikizaji, na wengi wao hawana uwezo wa kuongea kutokana na uwoga wa natukio mabaya waliy yaona na kutendewa mbele ya macho yao, na wengine hawajuhi kama wazazi wao bado wanaishi.

“Ili kufikiria jambo hili ya kwamba ni jambo la kipeo kikubwa cha wakimbizi huko afrika , hawali ya yote ni kuwaza kwamba ni zaidi ya milioni moja na nusu ya watu walio kimbia kutoka Sudan ya kusini baada ya mlipuko wa vita tangu Decemba 2013 .Mwaka jana watu walio tokea Sudan ya kusini kupitia Uganda walikuwa idadi kubwa kuliko wakimbizi walio pitia bahari ya meditrenia kwa kipindi kama hicho.Anasisitiza  maneno hayo Valerio neri ,Mkurugenzi wa Save the Children.Ushuhuda wa ukatili wa nguvu  unatolewa na baadhi ya watu ambao wameona ndugu zao, mama zao , au marafiki zao wanauwawa , kinyama hadi kunyongwa na makundi hayo ya kikatili.Watoto wengi hawawezi kusimulia vitendo vya kikatili walivyo viona kwa macho yao au kutendewa kwani ni vitendo vya kutisha. Peter Walsh Mkurugenzi wa Save the children huko Sudan ya Kusini anasema wana wasiwasi mkubwa kama   Umoja wa Mataifa  hawaingilii kati juu  mauaji hayo ya Suda ya Kusin.Anatoa wito kwa sehemu zote mbili za zenye migogoro kuwalinda raia kwasababu shuhuda nyingi  zinazosikika , ni za kutosha . Watoto wanafika wakiwa peke  yao wamelazimika kuacha nyumba zao ili kutafua mahali penye ulinzi na usalama, na wengi wao wamekonda kwa sababu ya njaa. Anaongeza kusema Save the Childreni imejikita katika kufanya kazi kwa ajili ya sudan ya kisin na kuwasaidai wakimbizi huko Uganda.Sehemu zote za migogoro wanapaswa kuhakikisha ulinzi wa raia aa hata wahudumu wa kibinadamu ili wapate kuendelea kutoa huduma muhimu za afya na ulinzi na zaidi kwa ajili ya watoto, anamaliza Walsh.

Hayo yote ni kutokana na ongezeko kubwa katika ukiukwaji wa haki za binadamu huko Sudan Kusini katika miezi tisa iliyopita na sehemu ni kutokana na kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kuunda mahakama na kuwafikisha wakosaji mbele ya sheria .Ukubwa wa ukosefu wa haki za binadamu huko Sudan Kusini hasa ghasia za ngono ni mbaya sana kiasi kwamba matokeo ya kutofanya lolote huwezi hata kufikiria yatakuwaje"hayo yalisemwa na Yasmin Sooka katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa huko Geneva siku ya Jumanne 14 Februari 2017 kwamba raia wamekuwa wakilengwa kimfumo kwa minajili ya kabila zao na serikali ya nchi hiyo na majeshi yake. Pamoja na hayo anasema,serikali imeanza kampeni ya kufuatilia wakazi na kuwafuatilia watu kutokana na kabila zao wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea huku kukiwa na maonyo ya mauaji ya halaiki

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.